Daily Archives: February 1, 2019

MADIWANI WA WILAYA YA CHAKE CHAKE KISIWANI PEMBA WAMETAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO

Madiwani wa wilaya ya chake chake  Kisiwani Pemba Wametakiwa Kutekeleza Majukumu yao kwa kufuata  Misingi ya Uatawala Bora  kwa Kuwashirikisha  Wananchi katika kuibuwa Miradi Itakayowaletea Maendeleo.

Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri  Ofisi ya Rais,KatibaSheriaUtumishi wa  Umma na Utawala Bora Mh.Khamis Juma Maalim  wakati alipokuwa akifunguwa kikao cha siku moja kilichowashirikisha  Madiwani wa Wilaya ya Chake pamoja na Watendaji wa Baraza la Mji  Chake.

Mh.Naibu Waziri amesema  Misingi ya  Utawala Bora inamfanyakiongozi  kuweza kutekeleza vizuri  Majukumu  yake  hivyo amewataka  Viongozi  hao kutekelza Misingi ya Utawala Bora  ukiwemo Sula Zima la Uwajibikaji.

Nae Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mh.Joji kazi amesema Kiongozi anatakiwa kutumia  Nguvu alizopewa  kisheria   kwa kuwatumikia Wananchi.

Mapema akizungumza  katika kikao  hicho Ofisa Mdhamini Ofisi ya Rais katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Nd.Massoud Ali Mohammed  amesema Lengo la kikao hicho ni kuweza kukumbushana  juu ya utekelzaji  wa Dhana ya Utawala Bora  ili kuweza kuapata  Maendeleo Endelevu.

Akiwasilisha Mada  ya Utawala Bora  katika kikao hicho  Mwanasheria kutoka Idara ya Utawala Bora   Hassan Vuai  Amesema Mashirikiano  ya Pamoja Ndio  yatakayopelekea Kufikia Malego ya Utawala Bora.

MAREKANI NA CHINA KUJIPA MATUMAINI YA KUWEZA KUTULIZA MVUTANO WAO

Marekani na China Wanaonyesha Kujipa Matumaini ya Kuweza Kutuliza Mvutano wao wa Kibiashara. Rais wa Marekani Donald Trump amesema baada ya Mazungumzo pamoja na Makamo wa Rais wa China Liu He,"makubaliano muhimu ya kibiashara yatafikiwa."Mjumbe wake katika mazungumzo ya biashara pamoja na China, Robert Lightizer amesema pia "maendeleo yameweza kupatikana" wakati wa mazungumzo yao. Rais Xi Jinping wa China ameandika katika risala yake anataraji pande hizo mbili zitaendelea kushirikiana katika hali ya kuheshimiana. Pindi makubaliano yakishindwa kufikiwa hadi Machi mosi inayokuja, rais Trump anapanga kuzitoza ushuru wa asilimia kati ya 10 na 25 bidhaa zote zitakazoingia Marekani kutoka China.

MAJAJI NA MAHAKIMU WANATAKIWA KUENDESHA KESI KWA HARAKA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mhe, Haroun Ali Suleiman amewataka Majaji na Mahakimu Kuendesha Kesi kwa Haraka ili Wananchi WawezeKupata haki zao katika kipindi  kifupi.

Amesema kufanya hivyo Itaonyesha Uwajibikaji wa Haraka katika Utekelezaji wao wa usimamizi waSheria katika kuwapatia haki kwa wananchi na hivyo wananchi kujenga imani na tasisi hiyo

Akifungua Maonesho yaMaadhimisho ya Sku ya Sheria huko Gombani Chake Chake, Mhe Haroun amewahimiza Wananchi kuyatumia Maonesho Hayo kwa kujifunza na kufahamu Taratibu Sahihi za kujua haki zao na jinsi ya kuzipata.

Amesema Fursa hiyo Iitumiwe na Majaji na Mahakimu  kuwashauri wananchi katika Kutatua Matatizo yao kwa kushirikia na sekta  ya Sheria ili kujuwa Njia za kuyatatua bila ya kuwepo kwa migogoro.

Aidha Mhe, Haroun Amekemea Vitendo vya Unyanyasaji Vinavyojitokeza kila siku hasa kwa Watoto na kuwahimiza Mahakimu kuangalia Sheria  na kuzitumia kwa Kuviangamiza Vitendo hivyo.

Akizungumzia Maonesho hayo Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu Amesema Maonesho hayo kufanyika Pemba ni Utekelezaji wa Agizo la Rais Dk. Shein kuitaka mahkama kuyafanya kisiwani humo ili wananchi wanufaike baada ya kufanyika kisiwani unguja takribani mara mbili.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdalla kwa Niaba ya Wananchi amesema maonesho kufanyika Gombani ni moja ya Mafanikio na Mashirikiano kati ya Tasisi za Umma na Jamii.

 

MASHUA YA PLASTIKI IMEIWEKA ZANZIBAR KATIKA RAMANI YA DUNIA

 

Ujio wa Mashua ya Mazingira Iliyotengenezwa kutokana na Malighafi ya Plastiki kutoka Nchini Kenya Chini ya Ushauri wa Taasisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa unaiweka Zanzibar katika Ramani ya Dunia kwenye Mapambano yake Dhidi ya Uchafuzi wa Mazingira.

Mashua hiyo ambayo tayari imeshaondoka jana kutoka mombasa nchini kenya inaingia Wete Kisiwani Pemba, kupitia Mkoani Pemba, Nungwi Mkoa Kaskazini Unguja na kutarajiwa kuingia  Forodhani Mjini Zanzibar mnamo tarehe 6 mwezi huu.

Kikao cha Washirika wanaosimamia na kushughulikia masuala ya Mazingira kutoka Taasisi za Umma, Binafsi pamoja na zile za Kimataifa  walikutana kujadili ujio wa Mashua hiyo chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdullah Hassan Mitawi kilichokutana Vuga Mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar Nd. Juma Mjaja aliwaelezea Wajumbe wa Kikao hicho kwamba lengo la Mashua hiyo ni kuihamasisha Jamii juu ya kuelekeza nguvu zao katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira yanayoleta Mabadiliko ya Tabia Nchi Duniani.

Nd. Mjaja alisema Tarehe 7 Febuari siku Moja baada ya kuwasili Mashua hiyo kutakuwa na uzinduzi wa usafi wa Mazingira katika Ufukwe wa Forodhani utakaoshirikisha Taasisi tofauti zinazojishughulisha na masuala ya Mazingira Zanzibar.

Naye kwa upande wake Ofisa wa Uratibu katika masuala ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bibi Clara Makenya alisema usafishaji wa Mazingira katika Pwani ya Forodhani itaongozwa na Muungano wa Taasisi za Kimazingira ya Les Do It Company Zanzibar.

Powered by Live Score & Live Score App