Daily Archives: February 4, 2019

JUMUIYA YA ZEDO YATAKIWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA NCHI

Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mh Hemed Suleiman Abdallad ameitaka Jumuiya ya maendeleo ya kielimu Zanzibar  zedo kufuata sheria na kanuni za nchi katika utoaji wa mikopo kwa wajasiri amali ili kuweza kuepukana na migogoro kati yao na wajasiri amali hao.

Mh Hemed ameitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa wanachama wa zedo ambao ni wajasiri amali  juu ya uchukuaji  mkopo wa chap chap huko katika ukumbi wa Samail Gombani chake chake pemba

Mh Hemed amesema ni lazima kwa jumuiya au taasisi kufuata sheria na kanuni ili kuweza kuondoa ubabaishaji  kwa wanachama wake sambamba na kuwataka wanachama hao kuitumia mikopo watakayoipata katika kupambana na umasikini na kijienua kiuchumi pamoja na kuwataka kurejesha mikopo hiyo kw awakati ili kuweza kutoa fursa kwa wanachama wengine kupata mikopo hiyo

Nae  mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo ya elimu Zanzibar  zedo ambae pia ni mkurugenzi wa mfuko wa mikopo nd ussi said suleiman amesema zedo imeanzisha mkopo wa chap chap kwa ajili ya wajasiri amali wadogo wadogo ili kuweza kuendeleza shughuli zao

Nao wanachama wa zedo ambao ni wajasiri amali wameziomba taasisi za kifedha zikiwemo bank kuweza kupunguza masharti ya uchukuaji wa mikopo kwa wajasiri amali wadogo wadogo .

 

MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA LINALOTAJIWA KUFANYIKA HAPA NCHINI YANZIDI KUPAMBA MOTO

Maandalizi ya Tamasha la Pasaka linalotajiwa kufanyika hapa nchini yanzidi kupamba moto huku waimbaji wengi kutoka nje ya nchi wakitarajiwa kushiriki tamasha hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa msama Promotion Alex Msama amebainisha hilo mbele ya waandishi wa habari kwa kusema kuwa waimbaji wa ndani watakaoshiriki tamasha hilo hawatazidi saba (7), lengo likiwa ni kuhakikisha wanapata fursa ya kuwa na idadi kubwa ya waimbaji kutoka nje.

Na katika kusisitiza shariti     la kusajiliwa kwenye baraza la sanaa la taifa basata kwa wasanii watakao shiriki tamasha hilo, Mkurugenzi Msama amesema wasanii  ambao wanadaiwa malimbikizo ya ada na basata, wamepewa fursa ya kufika Msama Promotion ili waweze kupatiwa fedha zitakazowasaidia kulipa madeni hayo, na kukidhi sharti la kushiriki.

Aidha Msama ametoa usahuri kwa basata kuwachukulia sheria wasanii wote wankiuka sheria, kanuni na taratibu za chombo hicho.

Kauli mbiu ya tamasha hilo, linalotarajiwa kuanza april 21, 2019ni umoja na upendo hudumisha amani ya nchi yetu.

SEKTA ZILIZOGATULIWA KUSINI PEMBA ZAKABILIWA NA MATATIZO YA WAFANYAKAZI NA VITENDEA KAZI

Wafanyakazi wa sekta zilizogatuliwa Mkoa wa kusini Pemba wamesema wanakabiliwa na matatizo ya wafanyakazi na vitendea kazi hivyo wameiomba serikali kuwatatulia matatizo hayo ili kufanikisha majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Hayo wameyasema kwa nyakati tofauti mbele ya Waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz mheshimiwa Haji Omar Kheir kwenye mikutano ya kusikiliza matatizo yanayozikabili sekta zilizogatuliwa  kisiwani Pemba

Wamesema katika kuona maendeleo yanazidi kuimarika ni vyema kwa serikali kubuni nafasi zaidi za ajira na kuzitafutia ufumbuzi  changamoto ndogo ndogo zilizopo.

Katika ziara hiyo waziri afisi ya rais tawala za Mikoa serikali za mitaa na idara maalum za SMZ mheshimiwa Haji Omar Kheir amesema kwa kushirikiana na viongozi wengine watakaa kuyafanyia kazi matatizo yaliopo ili kuona sekta hizo zinasonga mbele kama ulivyo mpango wa serikali wa kuwaletea wananchi wake huduma karibu nao .

Amesema katika  kuimarisha dhana ya ugatuzi  serikali imepanga katika  bajeti ya  2019-2020 kujenga madarasa 600 unguja na Pemba ili kukidhi haja ya ukosefu wa vyuma vya kusomea

Mapema Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla amewataka wafanyakazi hao kuzidi kujituma huku serikali ikiendelea kuzitafutia ufumbuzi wa kina changamoto zao.

Powered by Live Score & Live Score App