Daily Archives: February 8, 2019

HALI YA USAFI KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MJI WA ZANZIBAR YAMEKUWA HAYARIDHISHI

Hali ya Usafi Katika Baadhi ya Maeneo ya Mji wa Zanzibar Yamekuwa Hayaridhishi Kutokana na Baadhi ya Watu Kupinga Sheria ya Utunzaji wa Mazingira.

Hayo Yamebainika BaadaKufanya Zoezi la Usafi wa Mazingira katika Maeneo ya Fukwe za Bahari ya Forodhani Ambapo Baadhi ya Wadau wa Mazingira Wamesema Kuendelea kwa Uchafuzi wa Mazingira Kunaweza Kutahatarisha Maisha ya  Wanadamu na  Viumbe Wengine wa Baharini.

Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi Marina Joel Thomas  Amesema si Vyema kwa Wanachi Kufanya Uchafu  Hasa katika Maeneo ya Fukwe za Bahari  Ambapo Kufanya  Hivyo Kunaweza  Kupunguza Idadi ya Watalii Wanaoingia  Nchini na Kuikosesha Serekali  Mapato.

Akizungumzia Juu ya Ujaji wa Boti  Iliotengenezwa  kwa Malighafi ya Plastik Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Mjini Nd Saidi Juma Ahmada  Amewataka Wananchi kuwa na Tabia ya Kuiga Mambo  ya Maendeleo .

Zoezi Hilo la Usafi wa Mazingira katika Maeneo ya Fukwe Yamewashiriksha Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Serekali, Washiriki Kutoka Kampuni ya Danause na Watendaji wa Serekali.

WANANCHI WAMEISHUKURU SERIKALI KWA UJENZI WA BANDA LA KUSUBIRIA WAGONJWA

Wananchi Kutoka Maeneo Mbali Mbali Wameishukuru Serikali Kupitia Wizara ya Afya kwa Ujenzi wa Banda la Kusubiria Wagonjwa Katika Hospitali Kuu ya Mmnazi Mmoja.

Wakizungumza kwa Nyakati Tofauti Wananchi Hao Wamesema Kumalizika kwa Ujenzi Huo Kutawawezesha Kukaa Katika Eneo Yenye Stara Tofauti na Sasa Ambapo Wanakaa Sehemu Yoyote Wakisubiri Muda wa Kuangalia Wagonjwa.

Akizungumza na Zbc Msemaji wa Hospital  Hiyo Hassan Makame Mcha   Amesema Wamelazimika Kujenga Banda Hilo Kutokana na Malalamiko ya Wananchi Wanaokuja Kusubiri Wagonjwa wao Ambao Hulazwa  katika Hospitali Hiyo Ambapo Wengi wao Wanatoka Maeneo ya Nje ya Mji.

Amesema ujenzi huo utakapo Malizka Kutakuwa na Maeneo aalum ya Kulala Watu wanaosubiri wagonjwa wao na kuondoka na hali iliyopo hivi sasa kulala katika wodi wakati unapokuwana wagonjwa.

Amesema Ujenzi Huo Unatarajiwa Kumalizika Mwezi Ujao Umegharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 30 na Utachukua Wananchi Zaidi ya 150.

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA IMESEMA IMEJIPANGA KUHAKIKISHA SUALA LA WAHAMIAJI HARAMU

Idara ya UhamiajiTtanzania imesemaIimejipanga Kuhakikisha Suala La Wahamiaji haramu wanaoingia Nchini Kinyume na Utaratibu wa Kisheria wa Uhamiaji Wanadhibitiwa.

Tamko hilo limetolewa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala wakati Alipotembelea Bandari Ndogo yaMkokotoni Kkaskazini Unguja,ambayo Inatumika Zaidi kwa Wasafiri Kutoka Tanga.

Amesema Ushirikiano Kati ya Wananchi Idara ya Uhamiaji Pamoja na Vyombo Vyengine vya Ulinzi na Usalama Utaongeza Nguvu za Kuweza Kudhibitiwa Wahamiaji Haramu Ambao Baadhi yao Wamekuwa Wakijihusisha ni Vitendo vya Kihalifu.

Akionesha Msisitizo juu ya Udhibiti wa Wageni Wanaoingia Kinyume na Sheria za Uhamiaji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Jumanne Tabaran Mzee, Amesema Wamekuwa na Mkakati wa KukabilianaVyema na Hali Hiyo.

Ziara hiyo Imeendelea kwa Kukagua Ofisi za hamiji Kinduni, Uunga Wilaya ya Kati na Ofisi ya Wilaya iliyopo Makunduchi.

VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUANZISHA VIPINDI VINAVYO HAMASISHA KUSOMA

Waziri wa elimu mafunzo ya amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma amewataka wamiliki wa vyombo  vya habari  kuanzisha vipindi  vinavyo hamasisha kusoma na sio kutoa burudani pekee.

akizungumza katika uzinduzi wa kapmeni ya tukutane skuli   amesema wasikilizaji na watazamaji wakubwa ni wanafunzi hivyo ni vyema kwa wamiliki wa vyombo hivyo kutoa vipindi vya elimu ili ufaulu wa wanafunzi uzidi kuongezeka.

mkuu wa mkoa wa mji maghribi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud amekipongeza kituo cha *zenji media group* kwa kuanzisha kipindi cha *tukutane skuli* ambacho kitawasaidia wanafunzi kujua wajibu wao katika kutafuta elimu.

nae meneja wa mradi wa *tukutane  skuli* Ndg.Yussuf Mohamed amesema iegno la kuanzisha kipindi hicho ni  kuwashajiisha vijana  hasa wanafunzi kuweza kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao.

 

Powered by Live Score & Live Score App