Daily Archives: February 11, 2019

ZAIDI YA WATU 500 WAFA KWA EBOLA DRC

Wizara ya afya nchini jamhuri ya kidemokrasi ya kongo imesema imefika zaidi ya watu 500 waliofariki kutokana na virusi vya ebola. Taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana imeeleza kuwa tokea kuibuka kwa ugonjwa huo mashariki mwa kongo, watu 505 wamekufa, na watu 271 wametibiwa. Ugonjwa huo ulizuka mwezi juni mwaka jana muda mfupi baada ya serikali ya nchi hiyo kutangaza kumalizika kwake katika eneo la magharibi mwa kongo. Kwa mujibu wa waziri wa afya wa nchi hiyo, oly kalenga, amesema tangu mwezi agosti, zaidi ya watu 70 elfu wamepatiwa chanjo ya ebola. Maafisa wa afya na mashirika ya kutoa misaada wamekuwa wakikabiliwa na matatizo katika kupambana na ugonjwa huo ikiwemo makundi mbali mbali ya wapiganaji yanaendesha operesheni zake, yakiwa yanagombania rasilimali za taifa hilo.

UKOSEFU WA HUDUMA YA UMEME KATIKA KIJIJI CHA KOKOTA

Wakaazi wa  kokota wilaya ya wete wamesema  ukosefu wa huduma ya umeme katika kijiji hicho  unarejesha nyuma jitihada za kupambana na umasikini na kujiimarisha kiuchumi.

Kauli hiyo wameitowa  wananchi hao  mbele ya wajumbe wa baraza  la kuwawakilisha watumiaji wa maji na nishati   katika muendelezo wa ziara ya baraza hilo  ya kusikiliza  changamoto  na maendeleo  yaliyopatikana ya upatikanaji wa maji na nishati.

Wamesema    kukosekana  kwa huduma ya umeme katika kijiji hicho  ni changamoto  inayopelekea  kuanguka kimapato  .

Wakizungumza  katika mkutano huo  makamo mwenyekiti wa baraza la wawakilishi wa watumiaji wa maji na nishati  bi fatma hamza amir na katibu wa  baraza hilo ahlam saleh khamis wamesema baraza linaendelea  na mpango wake wa kukusanya  maoni ya wananchi ili kuweza kuziwasilisha kunakohusika  kwa kupatiwa ufumbuzi ili wananchi nao waweze kufaidika na huduma  muhimu za kimaendeleo.

 

KAMATI ZA KUKABILIANA NA MAAFA WILAYA YA CHAKE CHAKE KUANDAA MPANGO MADHUBUTI

Afisa mdhamini ofisi ya makamu wa pili wa rais  nd.ali salim mata  amezitaka kamati za kukabiliana na maafa wilaya ya chake chake  kuandaa mpango  madhubuti  utakaowawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi   na kuepusha migongano wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Kauli hiyo ameitowa wakati alipokuwa akifunguwa mafunzo ya siku mbili  kwa kamati za kukabiliana na maafa  wilaya yachake chake  huko katika ukumbi wa tassaf.

Nd.mata amesema mpango madhubuti  wa kukabiliana na  maafa  utapelekea kuweza kuwanususru wananchi   na mali zao  hivyo ni vyema kwa  kamati kuona umuhimu wa mpango huo pamoja na kuweza kuendelea kushirikiana kwa kufikia malengo .

Nae naibu mkurugenzi wa kamisheni ya kukabilina na  maafa nd. Muhidini  ali muhidini amesema umuhimu wa mpango huo ni kuleta  ufahamu  na ufanisi  zaidi katika kutekeleza majukumu yao sambamba na  kuzitaka kamati kuwafikishia elimu  ya maafa wananchi  ili kuweza kujikinga  na maafa .

Mapema akizunguma katika mafunzo hayo kaimu mratibu wa kukabiliana na maafa  pemba nd.mbela issa mbela amewatka  wanakamati  hao kuweza kushiriki  kwa kutoa maoni yao  kwa kuandaa mpango huo  kwa kuangalia  mazingiara halisi ya meneo yao.

Katika mafunzo hayo ya siku mbili  yaliyowashirikisha wanakamati  wa  kukabiliana na maafa wiilaya ya chake chake  ambapo mada mbali mbali zilijadiliwa  lengo likiwa  ni kuandaa mpango wa kukabilina na maafa katika  wilaya hiyo.

 

WANANCHI WETE WANAKABILIWA NA TATIZO LA MAJI SAFI

Wananchi wa shehia ya fundo wilaya ya wete wamesema wanakabiliwa na tatizo la maji safi  katika kisiwa hicho hali inayowapa usumbufu katika shughuli zao za kimaisha.

wakielezea changamoto na matatizo yanayohusu upatikanaji wa maji na nishaji, wamesema miundombinu mbinu ya usambazaji wa maji ipo lakini huduma ya maji hupatika katika vijiji viwili tu kwa baadhi ya siku na hutoka usiku mkubwa.

Wananchi hao wametowa malalamiko hayo mbele ya wajumbe wa baraza la kuwawakilisha watumiaji wa maji na nishati walipowatembelea katika shehia yao.

Wakitowa ufafanuzi wa maoni ya wananchi hao, mwenyekiti wa baraza hilo mahmoud mohamed mussa na makamo mwenyekiti fatma hamza amir wamekiri kuwepo kwa tatizo la upatikana wa maji katika wilaya hiyo na kwamba lipatiwa ufumbuzi kwani baraza hilo lipo kwa ajili ya wananchi.

 

 

 

Powered by Live Score & Live Score App