Daily Archives: February 14, 2019

DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEWATAKA WANANCHI WA KIANGA KUKITUMIA IPASAVYO KITUO CHA AFYA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi wa shehiya ya Kianga, Wilaya Magharibi 'A' kukitunza vyema pamoja na kukitumia ipasavyo kituo cha Afya, ili kiweze kuwa endelevu na kuleta tija kwa jamii.

Dk. Shein amesema hayo leo katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la msingi la Kituo cha Afya Kianga, kilichojengwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa mashirikiano na wananchi.

Alisema suala la upatikanaji wa huduma bora za Afya nchini halina mbadala, hivyo kuna haja ya kukitunza kituo hicho na kuhakikisha wananchi wa shehiya hiyo na nyengine jirani wanafika kupata huduma.

Alisema pamoja na wananchi kuendelea na tamaduni za kupata huduma za afya kupitia njia za jadi, kuna umuhimu mkubwa wa kukitumia ipasavyo kituo hicho, ambacho kitaendeshwa kupitia afya ya msingi chini ya mfumo wa Ugatuzi.

"Sisemi yale ya asili msifanye, sijasema hivyo yale fanyeni lakini pia hospitalini mje............, sitaki kuondosha imani za watu", alisema.

Aidha Dk. Shein aliiagiza Wizara Afya kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya Magharibi "A" kuhakikisha kituo hicho kinakuwa katika mazingira bora, ikiwa pamoja na kukipatia wataalamu wa kukihudumia.

Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwapongeza wnanachi wa Kianga kwa uamuzi wao uliolenga kupatiwa huduma za afya, ili kuondokana na kadhia ya muda mrefu ya kufuata huduma hizo katika vituo vya afya vilivyopo masafa marefu.

Akigusia historia ya huduma za Afya nchini, Dk. Shein alisema Mapinduzi ya 1964 yamekuja kuwakomboa Wazanzibari wanyonge kuondokana na kadhia ya kukosa huduma bora za afya.

Alisema kabla ya Mapinduzi, huduma za Afya (kama ilivyo kwa elimu), zilitolewa kwa misingi ya ubaguzi kuambatana na uwezo wa mtu, hivyo Wazanzibari walio wengi walikosa huduma hiyo muhimu.

Katika hatua nyengine Dk. Shein aliwapongeza watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Zanzibar, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais  pamoja na wananchi wote waliofanikisha ujenzi wa kituo hicho.

Mapema, Waziri wa Nchi, (OR), Tawala la Mikoa na Serikali za Mitaaa na Vikosi vya SMZ, Haji Omar Kheir alipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli za kuimarisha mfuko huo kifedha kupitia Benki ya Dunia (World Bank).

Alisema ni haki ya wana CCM kuendelea kutembea kifua mbele, kutokana na mafanikio makubwa yaliopatikana katika  utekelezaji wa Ilani ya CCM, kupitia sekta tofauti ikiwemo Afya.

Waziri Kheir, aliahidi kushirikiana kikamilifu na Wizara ya Afyana kuandaa mikkakati  ili  kupata wataalamu bora wa kukiendeleza kituo hicho.

Nae, Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mihayo Juma Nhunga, alisema kukamilika kwa ujenzi huo kutawaondolea usumbufu wananchi wa Kainga wa kufuta huduma za Afya katika vituo vya Kizimbani na Bumbwi sudi.

Alisema hatua hiyo itafungua milango ya maendeleo kwa wananchi wote wa Jimbo la Mwera.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu, (WN) Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Abdalla Hassan Witawi, alisema ujenzi wa kituo hicho ulioanza Julai, 2018 umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 104 hadi sasa, ukifikia asilimia 85 ya ujenzi wote.

Mitawi alizipongeza Ofisi za Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, na Wilaya Magharibi 'A' pamoja na Kamati ya Uongozi wa Shehiya ya Kianga kwa mashirkiano yao yaliofanikisha vyema ujenzi wa kituo hicho

Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein aliendelea na ziara yake kwa uzinduzi wa kituo cha kukaushia Dagaa, huko Kihinani.

Akizungumza na wananchi na wajasiriamali baada ya kukaguwa mashine ya kukaushia dagaa, Dk. Shein aliwataka wajasiriamali hao kuendelea na shughuli zao na kuuza bidhaa zilizo bora ndani na nje ya nchi bila ya woga.

Alisema Zanzibar imebarikiwa kuwa na bahari yenye rasilimali kadhaa, hivyo ni vyema ikatumika katika kuwakomboa wananachi kuoka katika lindi la umasikini, akiwashauri kuuza bidhaa hizo hadi Kongo na Malawi ambako soko kubwa hupatikana.

Aliitaka Wizara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi, kubuni njia bora zaidi ili kuwawezesha wajasiriamali na wafanyabiashara wa dagaa waweze kutumia mbinu bora za ukaushaji ili waweze kuzalisha bidhaa bora na kukidhi soko la nje ya nchi.

 

Aidha, Dk. Shein aliwataka wajasiriamali hao kuwa makini katika matumizi ya mashine hiyo wakati wa ukaushaji ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza na kuharibu ubora wa bidhaa zao.

Alisema serikali inaendelea na juhudi za kuimarisha sekta ya uvuvi kwa kununua meli mbili mpya, sambamba na kulifufua shirika la ZAFICO , azma inayokwenda sambamba na ujenzi wa viwanda vya Mwani, kwa mashirkiano na washirika wa maendeleo.

Dk Shein, aliwapongeza wananchi hao kwa utulivu na usikivu wao wa kukubali kuhama katika eneo la Maruhubi walipokuwa wakiendesha shughuli hizo na kuhamia Kihinani.

Mapema, Waziri wa Nchi (OR) Tawala na Mikoa, Serikali za Mitaa na Vikosi vya SMZ, Haji Omar Kheir aliwapongeza wajasiriamali kwa kukubali agizo la Serikali la kuondoka Maruhubi na kuhamia Kihinani, kwa hiari.

Alisema Serikali haina lengo la kuwaonea wananchi wake, akibainisha kuwa utekelezaji huo unakwenda sambamba na Ilani ya CCM katika kuwawezesha wananchi kiuchumi.

"CCM daima itaendelea kuwajali watu wake na kuwa mtetezi wa wanyonge wa nchi hii", alisema.

Alisema imelenga kuliendeleza eneo hilo kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa Bandari ya kisasa, hatua itakayochangia ustawi mkubwa uchumi wa Taifa.

Nae, Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Magharibi 'A' Amou Ali Mussa alisema Bara hizo limetumia zaidi ya Shilingi Milioni 17.1 kwa ajili ya  kulipa fidia wananchi waliokuwa wakilitumia eneo hilo la Kihinani.

Alisema tayari wajasiriamali hao wameanzisha kikundi cha Ushirika ili kuwa na ngvu ya pamoja katika uendelezaji wa biashara zao, ambapo miongoni mwa changamoto zinazokabili ni ukosefu wa barabara za ndani.

Alisema bado Baraza la Manispaa linadaiwa kiasi cha shilingi Mklilioni 34, kukamilisha deni la fidia za wananchi.

Aidha, alisema kuna changamoto ya ufinyu wa nafasi kwa ajili ya wafanyabiashara, ambapo eneo la eka 1.3 limeazimwa kutoka Chuo cha Mwalimu Nyerere na hivi sasa linahitajika kwa matumizi ya chuo hicho.

Alisema kiasi cha wananchi 1,396 wananufaika kwa kuendesha shughuli za ujasiriamali mahali hapo.

Pia, Dk. Shein katika ziara hiyo, alikutana na Viongozi na wanachama wa chama hicho Jimbo la Mfenesini, katika mkutano uliofanyika Tawi la CCM Mtoni.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuzungumza na wanachama na kuangalia utekelezaji wa Ilani pamoja na changamoto zake.

Akizungumza na viongozi hao alisitiza haja ya wana CCM kushikamana na kushirikiana ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kushika Dola katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kukijengea uwezo chama ili kuwa  wanachama wengi ili waweze kukipigia kura na kuhsinda katika uchaguzi huo.

Alisema ushindi wa CCM katika uchaguzi huo hauna mashaka, lakini akawataka wana CCM kuongeza juhudi z za kukiimariksha ili kiweze kushinda kwa kishindo.

Alisema anatambua kazi kubwa aliyonayo katika kufanikisha ushindi huo na kuukabidhi kwa Rais ajaye.

Aidha, aliwataka Viongozi wa Jimbo hilo kukamilisha ahadi walizoweka kwa wananchi na kuwapongeza wale waliokamilisha ahadi hizo, akiweka bayana kuwa yeye tayari ametekeleza ahadi zote.

Katika hatua nyengine aliwataka viongozi na wanachama hao kuwaeleza wananchi yale yote yanayofanywa na Serikali ya CCM, ili kuepuka upotoshaji kutoka kwa viongozi wa upinzani.

Alisema serikali inaendelea na juhudi zake za kuimarisha sekta za kijamii, ikiwemo afya, elimu, maji na barabara

Nae, Katibu Mkuu wa CCM, Juma Abdalla Sadalla, alimhakikishiaa Dk. Shein kuwa utekelezaji wa Ilani unaendelea vyema, akisifu mashirikiano makubwa yaliopo katika ya viongozi wa Wizara za Serikali na Uongozi wa chama hicho.

Alisema juhudi zinaendelea kutoa mwamko kwa wanaachama wa chama hicho kupitia nyumba kwa nyumba ili kuwa katika mazingira bora ya uchaguzi wa 2020.

WATENDAJI WA SECTA YA ELIMU KUJADILIANA MAMBO WALIO KABIDHIWA KATIKA UGATUZI

Katibu  Mkuu ofisi ya Rais tawala za mikoa, Serikali za mitaa na idara maalum za SMZ Nd Radhiya Rashid  Haroub amesema ipo haja ya kukaa na watendaji wa secta ya elimu ili kujadiliana mambo walio kabidhiwa katika ugatuzi  ili kuondosha matattizo yanayoikabili secta hiyo.

ameyasema hayo katika kikao cha kujadili mkakati wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na upungufu wa wafanyakazi kwa mamlaka za serikali za mitaa katika ukumbi wa magereza.

amesema wamegundua kuwa skuli nyingi zina walimu ambao hawana sifa na kupelekea kukosekana kwa ufaulu kwa wanafunzi hivyo amesema wizara itahakikisha bajet iliyokuwepo inatoa ajira kwa walimu ili kuona ubora wa elimu unafikiwa nchini.

akitoa mada ya muelekeo wa bajet ya elimukwa mwaka 2019/2020 kwa ngazi ya elimu ya maandalizi na msingi mkurugenzi mipango sera na utafiti Nd Khalid Masoud Wazir amesema suala la uwandikishaji limekuwa kwa kasi kubwa kutoka asilimia 20 ya mwaka 2008 hadi kufikia 2018 kuna wanafunzi asilimia 47 nukta 6

nae mkurugenzi uwendeshaji Omar Ali Omar akitoa mada kuhusu mpango wa rasilimali watu katika elimu amesema wiazra ya elimu imeandaa mpango wa ajira wa miaka mitano kwa idara ya msingi na maandalizi kwa kwakuajiri walimu 40 wachetimwaka 2019/2020 nawalimuwa diploma 150

amesema ongezeko hilo limekuwa zaidi ya 2016 baada ya kutangazwa kufutwa kwa michango ya wazee na kuhakikisha wanafunzi wanapatiwa elimu bora

akichangia bajet hiyo mkurugenzi maandalizi namsingi Bi Safia Rijali amesema suala la upungufu wawalimu Nchini ni tatizo kubwa hasa kwa upande wa Pemba

Powered by Live Score & Live Score App