Daily Archives: February 15, 2019

DK.SHEIN AMESEMA KUANZISHA TAASISI ZA UTAFITI NI LENGO LA KUPATA UJUZI NA UFUMBUZI WA MAMBO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  ameeleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuanzisha taasisi za utafiti ikiwa na lengo la kupata ujuzi na ufumbuzi wa mambo mbali mbali ya kimaendeleo.

Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzbar wakati alipokuwa na mazungumzo na  Profesa Biang Yuhong Mtaalamu wa Utafiti kutoka Jamhuri ya Watu wa China aliyefuatana na mwanafunzi wake Siambi Kikete kutoka nchini Kenya pamoja na uongozi wa Wizara ya Afya.

Katika maelezo yake, Rais Dk. Shein alieleza kuwa katika kuhakikisha Zanzibar inaimarika kwenye suala zima la utafiti tayari imeshaanzisha Taasisi za Utafiti kwa lengo la kupata ujuzi na maarifa juu ya masuala mbali mbali yakiwemo masuala ya afya, kilimo na mifugo.

Aliongeza kuwa tayari Taasisi tatu za Utafiti hapa Zanzbar zimeshaanza kufanya kazi zake vyema ikiwemo Taasisi ya Utafiti wa Afya, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ambapo taasisi hizo zimeanza kazi vyema.

Rais Dk.Shein alieleza kuwa hatua hiyo ni juhudi na mikakati iliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzbar ya kuhakikisha suala zima la utafiti linapewa kipaumbele hapa Zanzibar.

Akieleza juu ya tafiti za dawa asili, Rais Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar ina umaarufu wa dawa hizo ambapo watu kutoka ndani na nje ya Tanzania waliitumia Zanzbar kama kituo cha dawa hizo.

Rais Dk. Shein alitumia fusa hiyo kutoa shukurani kwa Profesa Biang Yuhong kwa kuja Zanzibar  na kutembelea maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba akiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya.

Hivyo, Dk. Shein alimuhakikishia Profesa Biang Yuhong kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kufanya kazi na Taasisi ya “Intergrated Medicine”  ya Chuo Kikuu cha Tiba Asilia cha Tiangin

Aidha, Rais Dk. Shein ameeleza mashirikiano mazuri yaliopo kati ya Zanzibar na Jamhuri ya Watu wa China ambapo alieleza kuwa nchi hiyo imekuwa ikiendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo.

Alieleza kuwa kuja kwa Profesa huyo ambaye ni Mtaalamu wa utafiti hasa kwenye masuala ya dawa asili kutafungua milango ya mashirikiano kati ya pande mbili hizo katika masuala ya utafiti ambayo yana umuhimu mkubwa hasa kwa wakati huu uliopo.

Nae Profesa Biang Yuhong ameyasifu mazingira ya visiwa vya Unguja na Pemba ambavyo alisema vimejaaliwa kuwa na miti mbali mbali yenye kutumika kwa tiba asilia.

Alieleza kuwa katika ziara yake katika visiwa vya Unguja na Pemba amegundua utajiri mkubwa wa miti ya dawa asilia na kueleza kuwa iwapo mikakati maalum itawekwa katika kuhifadhi na kuitunza miti hiyo Zanzibar inaweza kuwa nchi maarufu kwa bara la Afrika na dunia nzima.

 

Alisema kuwa kuwepo kwa taasisi za Utafiti hapa Zanzibar zitaweza kuwa chachu katika kugundua dawa kadhaa hali ambayo itaendelea kuifanya Zanzibar iendelee kuwa kuwa kivutio kwa wageni kutoka nchi mbali mbali duniani.

 

Aidha, Profesa Biang Yuhong alimuhakikishia Dk. Shein kuwa Taasisi yake ya “Intergrated Medicine” ya Chuo Kikuu cha Tiba Asilia cha Tiangin iko tayari kushirkiana na Taasisi ya Utafiti ya Afya ya Zanzibar.

Mapema Mtaalamu wa Utafiti kutoka Kenya  Siambi Kikete alimueleza Rais Dk. Shein akiwa na Profesa huyo kutoka China wameweza kutembelea sehemu mbali mbali ikiwemo msitu wa Ngezi ambao una miti mingi yenye tiba asilia.

Alisema kuwa miongoni mwa miti hiyo ni pamoja na mti wa aina ya Aloe Pembana ambao haupatikani sehemu nyengine yoyote duniani isipokuwa katika kisiwa cha Pemba pamoja na mti wa aina ya Mjafari ambao unapatikana Pemba na Unguja pekee.

Aliongeza kuwa miti hiyo imeanza kupotea kutokana na wataalamu wa tiba asili kuitumia vibaya hivyo, alitoa rai ya kuenziwa na kuhifadhiwa kwa miti hiyo ili iweze kuwasaidia vizazi vilivyopo na vijavyo.

Aidha, mtaalamu huyo alitoa pongezi kwa Rais Dk. Shen kwa kuanzisha Taasisi za Utafiti ambazo alisema hatua hiyo mbali ya utaalamu utakaopatikana pia itakuwa ni chanzo cha kuimarisha na kuendeleza Utalii.

SMZ IMEANZA KUPOKEA VIFAA MBALI MBALI VYA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO NCHINI

Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar Imeanza Kupokea Vifaa Mbali Mbali vya Ujenzi wa Miundombinu ya Mawasiliano Nchini Ilivyovinunua kutoka Nchini Brazil na Italy kwa Ajili ya Kuimarisha kazi ya Utengenezaji wa Bara Bara Nchini katika Kiwango cha Kitaalamu Zaidi.

Asilimia Kubwa ya Vifaa Hivyo Vilivyoletwa Nchini karibu Mwezi Mmoja Uliopita Hivi SasaVimewekwa Katika Eneo la Kibele Vikisubiri Mtaalamu wa Kuvifunga ili Vifanyiwe Majario na Kuanza kazi Mara moja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akiwa  Pamoja na Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Mawaziri Alifika Katika Eneo la Kibele Kujionea Mwenyewe Vifaa Hivyo Vitakavyoleta Ukombozi Mkubwa kwa Idara ya Utunzaji na Utengenezaji Bara Bara Zanzibar {UUB }.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na UsafirishajiZanzibar Nd. Mustaha Aboud Jumbe Alimueleza Balozi Seif kwamba Awamu ya kwanza ya Vifaa hivyo ilitanguliwa na Mtambo wa kupikia lami ulionunuliwa na serikali kwa gharama ya Dola za Kimarekani Laki 937,000.

Nd. Mustafa Alisema Vifaa Vyengine ni Gari la kuchanganyia lami na kokoto, gari ya kutandaza lami ya moto pamoja na gari ya kutandazia lami Wakati wa Ujenzi wa Bara Bara.

Katibu Mkuu Huyo wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Alieleza Kwamba Awamu ya Pili ya Vifaa Hivyo Itakayojumuisha Pia Magari  Kumi Pamoja na Grader Vinatarajiwa Kusaili Nchini si Zaidi ya Mwezi Juni Mwaka Huu.

Naye Mkurugenzi Mkuu waIdara ya Utunzaji na Utengenezaji wa Bara Bara Zanzibar Nd. Ali Tahir Fatawi Alisema Mtambo Huo Ulionunuliwa kwa Kuzingtatia Hali Halisi ya Mazingira Nchini ni wa Pili Kununuliwa na Serikali Ambao Utasaidiana na Ule Unaotumika Hivi Sasa.

Nd. Tahir Alisema Wakati Mtazamo wa Wizara ya Ujenzi Kupitia Idara yake ya Utunzaji na Utengenezaji wa Bara Bara Umelenga Kununua Lami tni 1,000 Mafunzo Maalum ya Wafanyakazi kuweza kumudu kuviendesha Vifaa Hivyo vya Kisasa Yatatolewa.

Akitoa Shukrani Zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Alisema Wahandisi Pamoja na Wafanyakazi wa Idara ya Utunzaji na utengenezaji wa Bara Bara {  UUBb } kwa Sasa Hawatakuwa Tena na Visingizio vya Ukosefu wa Vifaa vya KaziWakati wa Kutekeleza Majukumu yao.

Balozi Seif  aAlitahadharisha Kwamba wakati Serikali Imejikita Kununuwa Vifaa Hivyo kwa Gharama Kubwa Wahandisi waUUB- Wanapaswa kuwa Makini na Kuacha Tabia ya Kujaribu Kubahatisha katika Matumizi ya Vifaa Hivyo Muhimu.

Nd. Mustafa Aliishukuru na Kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Jitihada Iiliyochukuwa Kuamua Kununua Vifaa  Hivyo Vitakavyolea Mabadiliko Makubwa ya Uwajibikaji kwa Watendaji wa UUB

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Chini ya Rais wake Dr. Ali Mohamed Shein Imenunuwa Vifaa Hivyo Vinavyokadiriwa Kugharimu Zaidi ya Shilingi Bilioni Tatu za Kitanzania ikilenga Kuimarisha Sekta ya Mawasiliano Hapa Nchini.

 

WANANCHI WA MBORIBORINI WANALIA NA MAJI YA ZAWA

Wanaanchi  wa  Shehia ya Mboriborini  Jimbo la Shaurimoyo  Wameendelea  Kuisisitiza Mamlaka ya Maji zanzibar (ZAWA) Kulifanyia  Matengenezo  ya Haraka Bomba   la Maji Ambalo Limekatika  na Kusababisha Huduma Hiyo  Muhimu Kupotea.

Wakizungumza na ZBC Wanaanchi Hao Wamesema   Kukatika kwa Bomba Hilo Kumesababisha  Kukosekana kwa Huduma Hiyo   Licha ya Wao Wenyewe  Kufanya Juhudi ya  Kujitolea  kwa Kuliziba  Bomba Hilo  Ili Maji Hayo Yasiendelee Kupotea Lakini  Wameonekana Kushindwa.

Wamesema  Pamoja na Kufanya Juhudi ya  Kutoa Taarifa juu   Kukatka kwa Bomba Hilo  Katika Mamlaka ya Maji Lakini Bado Hazijapatiwa Ufumbuzi Wowote  kwa  Muda Usiopungua Wiki ya Tatu Sasa Huku Wakaazi wa Maeneo ya Hapo Wakikosa Huduma Hiyo Kufuatia Bomba Hilo Kukatika.

Kwa Upande Wao Sheha wa Shehia ya  Mboriborini  Mzee Haji Mussa  na Mjumbe wa  Sheha  Salum Nassor Salum Wamesema   Walishauri  Kubadilishwa  kwa Mabomba Hayo Kutokana  na Yanayoumika Hivi Sasa  kuwa Yameshachakaa kwa Muda Mrefu Lakini Wanashindwa Kupata Ushirkiano  Kutoka kwa Mamlaka Hiyo.

 

WANANCHI WA KIJIJI CHA MAKAANI WAMETOA MASIKITIKO YAO KWA KUKOSA HUDUMA YA UMEME

Wananchi wa  Kijiji cha Makaani Shehia ya Kojani Wameelezea Masikitiko Yao kwa Kukosa Huduma ya Umeme Tangu Kupelekwa kwa Huduma Hiyo Katika Kisiwa Hicho  Kutokana na Nguzo Zao za  Umeme Kuchukuliwa na Kupelelekwa Eneo Lisilojuilikana na Kushindwa Kumudu Gharama za Ununuzi wa  Nguzo Hizo .

Wakitoa Malalmiko Hayo  Mbele ya Baraza  la Kuwakilisha Watumiaji wa Maji na Nishati  CRcC  Wamesema  Kuchukuliwa kwa Nguzo Hizo Kumesababisha Wananchi Hao kushindwa kujiletea mabadiliko ya kiuchumi.

Kwa  Upande Wake Mjumbe wa Baraza Hilo Ahlam Saleh Khamis Amesema Lengo la Kuundwa Baraza Hilo ni Kuskiliza Maoni  , Malalamiko  na Maombi ya Wananchi Nakuyawasilisha kwa Wahusika ili Kutatua Chanagamoto  Zao Katika Upatikakanaji Bora   wa Huduma za Maji na Nishati.

Powered by Live Score & Live Score App