Daily Archives: February 19, 2019

ROBO FAINALI YA MASHINDANO YA ZBC SPICE FM YAMLE YAMLE CUP IMETANGAZWA

Robo fainali ya mashindano ya zbc spice fm yamle yamle cup imetangazwa leo hii huku michezo yote hiyo minne ikitarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa polisi ziwani majira ya saa 10:00 za jioni.

Mchezo wa robo fainali ya kwanza itaanza kuchezwa alhamis ya feb 21, kati ya saccos fc kutoka potoa itakuwa na kazi kucheza na timu ya magari ya mchanga .

Ijumaa feb 22 kutakuwa na mchezo wa robo fainali ya pili kati ya bandari ya muwanda kucheza na  uzi city ya meli nne taveta ambapo

Jumamosi feb 23 juves camp kutoka daraja bovu watachuana na timu ya tra kutoka magomeni.

Na robo fainali ya mwisho itahitimishwa jumapili feb 24 kati ya tila lila fc kutoka fuoni wataonyeshana na kazi na hauto brazil kutoka amani.

 

PANDE HASIMU NCHINI YEMEN ZIMEKUBALIANA KUONDOA VIKOSI HODEIDA

Serikali ya yemen na wawakilishi wa wanamgambo wa kishia-houthi wamekubaliana kuhusu awamu ya kwanza ya kuwaondowa wanajeshi kutoka mji wa bandari wa hodeida na katika bandari za salif na ras isa. Umoja wa mataifa umesema hayo ni makubaliano muhimu yaliyofikiwa. Bandari ya hodeida ni muhimu kwani ndiko inakofikia misaada ya jumuia ya kimataifa kwa ajili ya wananchi kutokana na nchi hiyo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kuhamishwa wanajeshi wa pande zinazohasimiana kutoka mji wa hodeida ni kiini cha makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa desemba iliyopita nchini sweden.

WALIMU WA SKULI KUTUMIA ZAIDI ZANA NA VIELELEZO KATIKA KUFUNDISHA WANAFUNZI

Katibu mkuu wizara elimu na mafunzo ya amali dk idrissa muslim hija amesema wakati umefika  kwa walimu wa skuli kutumia zaidi zana na vielelezo katika kufundisha wanafunzi badala ya kutumia chaki, mdomo na ubao pekee.

Dk muslim amesema hayo wakati akisoma  hotuba ya waziri wa elimu na mfunzo ya amali  katika chuo kikuu cha taifa zanzibar (suza) kampasi ya nkrumah kwenye ufunguzi wa maonesho ya zana za kufundishia na kujifunzia  .

Amesema iwapo vitendea kazi na vielelezo vitatumika vizuri na kwa muda sahihi kuna uwezekano mkubwa kiwango cha ufahamu kwa wanafunzi kuongezeka na kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya taifa na kuinua kiwango cha elimu.

Mkuu wa skuli ya elimu ya suza dk. Maryam jaffar ismail amesema wanafanya juhudi ya kuwaandaa walimu wanaosoma chuoni hapo kutengeneza zana za kusomeshea kwa kutumia vitu vilivyopo katika mazingira yaliyowazunguka ambavyo havina gharama kubwa ili kuwasaidia wanafunzi wao na kuongeza ufanisi katika kazi hiyo.

Amesema changamoto inayoikabili kada ya elimu nchini ni vijana wengi kukataa kujiunga na kada hiyo na wanaojiunga ni vijana wanaokosa  masomo katika fani nyengine jambo ambalo alisema sio sahihi.

Katika risala ya walimu wanafunzi wa kada ya ualimu suza walisema wanakabiliwa na tatizo la sehemu ya kutengeneza zana za kufundishia na kujifunzia na sehemu ya kuzihifadhi baada ya kuzitengeneza hivyo wamekiomba chuo kutafuta sehemu maalum  kwa kazi hiyo.

 

ZANZIBAR KUNUFAIKA NA MIRADI YA UJENZI WA MABWENI KATIKA SKULI YA SEKONDARI

Zanzibar inatarajiwa kunufaika na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa mabweni katika skuli ya sekondari ya juma pindua kisiwani pemba pamoja na mradi wa usambazaji wa huduma ya usambazaji wa maji safi na salama katika jimbo la mwera miradi inayofadhiliwa na seriklai ya japan.

Utiaji saini mkataba wa mradi wa upanuzi wa mfumo wa usambazaji maji katika jimbo la mwera na wa ujenzi wa mabweni umekuja kufuatia maombi yaliyowasilishwa na viongozi wa serikali akiwemo mkamu wa pili wa raisi wa zanzibar  balozi seif ali iddi.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa katika hafla hio mradi wa usambazaji maji utagharimu shilingi milioni 188, na ujenzi wa mabweni utagharimu shilingi milioni 288 zinazotolewa na serikali ya japani kupitia mfuko wa misaada wa nchi hio.

Wakizungumza katika hafla ya utiaji iliofanyika katika makaazi ya balozi wa japani nchini tanzania, jijini dar es salaam naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili mh. Mihayo juma nhunga na naibu waziri wa elimu na mafunzo ya amali mmanga mjengo mjawiri wamesema utekelezaji wa miradi hio itasaidia kugfanikisha mipango ya serikali ya kuwafikishia wananchi huduma bora za kijamii.

Kwa upande wake mwakilishi wa taasisi ya maendeleo ya kupambana na umasikini amesisitiza haja ya wananchi kupata maji, kwa kusema kuwa msingi mzuri wa maendeleo ni upatikanaji wa miundombinu ya maji, afya, elimu usafiri na usafirishaji.

Balozi wa japani nchini tanzania balozi shinichi goto ameahidi kuwa serikali ya japani kupitia mfuko wa misaada itaendelea kutoa misaada ya mahitaji muhimu.

Mbali na miradi hio miwili, ya zanzibar  pia kulifanyika utiaji saini wa mradi wa ufungaji wa vifaa tiba katika vituo vya afya vya kirando na mawimbi vilivyopo mkoani rukwa ambapo jumla ya dola za kimarekani laki 2, 77 elfu , 445 ambazo ni sawa na shilingi milioni 615 zitagharimu ujenzi wa miradi hio.

Powered by Live Score & Live Score App