Daily Archives: February 20, 2019

MABARAZA YA VIJANA KISIWANI PEMBA KUTOKATA TAMAA

 

mwenyekiti wa baraza la  vijana  zanzibar khamisi rashid kheir makoti ameyataka mabaraza ya vijana kisiwani pemba kutokata tamaa kutokana na changamoto  zinazowakabili na badala yake  waongeze bidii  katika utendaji ili lengo lakuanzishwa mabaraza hiyo liweze kufikiwa.

makoti ameyasema hayo huko kwenye afisi za  baraza la vijana kibirinzi alipo kuwa akizungumza na wenyeviti na makatibu wa baraza ya vijana wilaya chake chake ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea harakati za vijana kisiwani pembamapema katibu wa baraza la vijana wilaya chake chake  bi stara khamis salim amesema bado kuna baadhi ya viongozi hawaja yapa mashirikiano mabarza ya vijana uwepo wake hata hivyo vijana wamekuwa mstari wambele katika kushirikiana na serekali katika harakati mbali mbali ndani ya wilaya chake chake

viongozi wa  mabaraza ya  vijana wilaya ya chake wameiomba serekali na tasisi binafsi kisiwani pemba kutumia  vijana waliyomo ndani ya baraza hayo katika kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na kuwapatia ajira   zamuda zinazo tolewa na serekali ikiwa pamoja na kazi za kupiga dawa za maleria tafiti ndogo ndogo kama vile takwimu kwa vile  mabara hayo yana vijana wenye sifa zote za kazi hizo

 

KMKM KANDA YA KASKAZINI KATIKA DORIA KUKAMATA POLO 436 ZA SUKARI ZIKITOKEA UNGUJA

Kikosi cha kuzuia magendo cha kmkm kanda ya kaskazini katika doria zake kimefanikiwa kukamata polo 436 za sukari zikitokea unguja kwenda tanga kwa ajili ya biashara.

Mkuu wa kamandi ya kmkm kanda ya kaskazi unguja  nd mohd mussa seif amesema imekuwa kawaida kwa baadhi ya manahodha wa vyombo hivyo kusafirisha bidhaa mbali mbali kwa njia hiyo huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Aidha amewataka wafanyabiashara na manahodha kufuata taratibu za usafirishaji wa bidhaa ili kuisaidia serikali kupata mapato yake na kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza.

Nae nahodha wa boti hiyo nd mohd ameir mnyimbo amewasihi manahodha wenzake kuacha tabia hiyo ambapo amesema inaweza kuwasababishia madhara makubwa katika maisha yao.

 

KUDHIBITI VITUO AU WATU WANAOFUNDISHA LUGHA YA KISWAHILI KWA WAGENI

Mkuu wa idara ya kiswahili kwa wageni chuo kikuu cha taifa zanzibar dkt. Zainab ali iddi ameiomba serikali kuwasaidia kudhibiti vituo au watu wanaofundisha lugha ya kiswahili kwa wageni bila ya kibali maalum kutoka  serikalini ili kudhibiti matumizi mabaya ya lugha ya kiswahili.

Dk zainab amesema hayo wakati akizungumza na zbc baada ya kusikiliza tafiti zilizowasilishwa  zilizowasilishwa na wanafunzi hao kutoka beijing nchini china wakiwa katika za mwisho za kumaliza masomo yao ya miezi minne ya kujifunza lugha ya kiswahili katika chuo kikuu cha taifa cha zanzibar.

Wanafunzi wanaojifunza lugha ya kiswahili katika chuo kikuu cha taifa zanzibar  kutoka beijing china wamesema zanzibar ni sehemu nzuri ya kujifunza lugha ya kiswahili kwani katika kipindi cha mienzi minne wamejifunza misamiati mingi ukilinganisha na miaka miwili waliyojifunza kiswahili wakiwa china.

Pia wanafunzi hao watano waliwasilisha tafiti zao walizozifanya kuhusu uchoraji wa tingatinga, mchango wa siti bint saad katika maendeleo ya taarab zanzibar ,utalii ni uti wa mgongo katika maendeleo ya taifa, na mlingano na tofauti baina ya majengo ya china na majengo ya zanzibar.

 

JUMUIYA YA MAGARI MAWE NA MCHANGA KUPELEKEWA HUDUMA MUHIMU KATIKA ENEO JIPYA

Jumuiya  ya magari mawe na mchanga wameiomba serikali kuwapelekea huduma muhimu katika eneo jipya walilohamishiwa huko jumbi ikiwa ni pamoja na kuwekewa kifusi ili waweze kufanya shughuli zao katika mazingira bora.

Kionozi wa Jumiya hiyo ndugu Hassan Ramadhan Kassu ameasema wamefarijika na hatua iliyochukuliwa na Serikali ya Mkoa  Mjini Magharibi ya kuwapatia eneo hilo badala ya Mwanakwerekwe, hata hivyo wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa huduma ya choo, maji na sehemu ya kuuza biashara  kwa kinamama.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mawe na mchanga wamesema hali ya biashara sio mbaya na wametoa wito kwa  wananchi  kufatia mahitaji yao katika eneo hilo na hakuna ongezeko lolote la bei.

Aidha wameiomba serikali kuruhusu tena uchimbaji wa mchanga, wamesema tangu kuzuiwa kwa uchimbaji wa mchanga biashara ya mawe imepungua pamoja na kuathiri ajira  za vijana wengi .

Wakati  huo huo wameiomba serikali kuzuia uchimbaji  wa mchanga kwa kutumia skaveta pale mchanga utakaporuhusiwa tena kuchimbwa kwani uchumbaji wake unaharibu sana  mazingira na kushauri kutumia uchimbaji wa zamani wa kutumia pauro.

Akielezea kuhusu changamoto zilizotajwa na wafanyabiashara ya mawe na mchanga Mkurugenzi Baraza la Magharibi B  Ndugu Ali Abdalla  Natepe amesema wanatambua uwepo wa kasoro hizo na wameanza kuchukua hatua ya kuzipatia ufumbuzi wake .

Amewataka wafanyabiashara hao waendelee kushirikiana na Baraza la Manispaa juu kuliimarisha eneo hilo.

Amesema pia suala la usafi wa maeneo hasa pembezoni mwa barabara litaendelea tena hivi karibuni katika njia mbalimbali za Manispaa hiyo na kutoa wito kwa watu walioweka magari mabovu  na majiko ya umeme, mafriji na bidhaa nyengine zilizotumika kuziondoa bidhaa zao ili kutoa nafasi ya kutumika vizuri barabara hizo.

Powered by Live Score & Live Score App