Daily Archives: February 21, 2019

WANANCHI WATAKIWA KUYADUMISHA NA KUYAENDELEZA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR.

Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi ambae pia makamo mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein amewataka wananchi kuyalinda kuyadumisha na kuyaendeleza mapinduzi matukufu ya zanzibar.

Akizungumza na viongozi na wanachama  wa chama cha Mapunduzi katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama hicho huko katika ukumbi wa mikutano residence hotel shehia ya kizimkazi amesema mafanikio yanayonekana sasa ya elimu, afya na maji ni sababu ya kujikomboa.

Aidha amewataka viongozi wote kukiimarisha chama cha Mapinduzi kwa kuwa karibu na wanachama majimboni na kuhakikisha wanatekeleza ahadi walizotoa sambamba na kufuata maadili na miiko ya uongozi ya chama na serikali ili waweze kurejeshwa tena na chama majimboni 2020.

Akizungumzia juu ya taarifa utekelezaji wa majukumu ya chama cha Mapinduzi na Serikali ya wilaya ya kusini amesema ameridhishwa na mafanikio yaliyopatikana na kuaahidi serikali kuondosha zile changamoto ndogo zilizopo kupatiwa ufumbuzi.

Waziri wa Nchi ofisi ya Raisi tawala za mikoa na idara maalum ya vikosi vya serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh: Haji Omar Kheir amewataka wananchi na viongozi kushirikiana na vikosi vya kuzuia magendo kmkm kwa kuwafichua wahalifu ili rasilimali za nchi ziwanufaishe na kuwasaidia wananchi wa zanzibar.

Naibu katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi Zanzibar Ndg. Abdallah Juma Sadala “mabodi” amewataka watu kukubali mafanikio yaliyopatikana na chama cha mapinduzi na serikali kwa ujumla kwani yanaonekana.

Akitoa neno la shukurani mkuu wa mkoa wa kusini Ndg. Hassan Khatib Hassan amepongeza Rais wa Zanzibar kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar na kueleza kua mafanikio yaliyopatikana yanatokana na kufanya kazi kwa kushirikiana sambamba na kuzingatia ilani ya chama cha Mapinduzi.

 

 

MILELE KUWASHAJIHISHA WATOTO WA KIKE KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

Taasisi ya milele zanzibar foundation katika mwaka huu imeendelea na lengo lao la kuwashajiisha watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi ili kupata vijana wasomi katika fani za sayansi kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani hali itakayosaidia kuinua uchumi wa nchi.

Akizungumza katika maadhimisho ya kutimiza miaka mitano katika pwani ya kizingo mkuu wa miradi  khadija sharif amesema   nchi nyingi duniani zinahamasisha kuweka safi mazingira ya bahari hivyo katika miaka mitano tasisi yake imejikita zaid kutoa elimu kwa vijana kujua matatizo yaloyopo katika sekta ya sayansi na  kuweza kuyatatua.

Nae alex moshi anaesimamia uchumi jamii katika taasisi hiyo amesema tasisi yake imesaidia mambo mengi katika sekta mbali mbali za elimu, afya uchumi jamiii, pamoja na kuinua kilimo kwa wakulima.

Mkufunzi kutoka suza zahor khamis amesema serikali zote mbili zinahamasisha uchumi  kupitia bahari hivyo ni vyema kuanzishwa uchumi wa blue kupitia bahari utawasaidia wananchi kuinua vipato vyao.

Skuli kumi na tano za ungj na pemba zimeshiriki katika ushafishaji wa mazingira, maonesho mbali mbali pamoja kupata mafunzo ya taaluma ya matumizi ya uchumi wa bahari.

ZANZIBAR KUSHIRIKIANA KIBIASHARA NA NCHI TOFAUTI

Zanzibar   hivi sasa  inaendelea   katika  masuala  ya kiuchumi   hivyo  ipo  haja  ya   kushirikiana kibiashara  na  Nchi  tofauti  ikiwa  pamoja na  uimarishaji wa  miundombinu ya  kibiashara ili  kuweza  kufikia adhma  hiyo .

Akizungumza katika  uzinduzi  wa maonesho ya  baadhi  ya bidhaa  za  india ikiwa  ni  miongoni  mwa  kukuza  uhusiano  wa  kibiashara  naibu  Waziri  wa biashara  na  viwanda  Mh  Hassan  Hafidh  amesema hali  hiyo  itasaidia  kurudisha  hadhi  ya  kibiashara  iliopo  awali   na  kuweza  kujiimarisha  zaidi  katika  uchumi  wa  viwanda ili  kufikia  uchumi  wa  kati.

Balozi  wa  india  Nchini  Tanzania bwana  Sandeep Arya amesema    Nchi  yake  imeamua  kutoa  upendeleo  maalu m  wa  ushuru   kwa  bidhaa   kwa  baadhi  ya  Nchi  ikiwemo  tanzania  pamoja  na  kufuta  gharama  za  viza  za  biashara kwa  wafanyabiashara wa  tanzania.

Nao  wafanyabiashara  waliohudhuriwa  uzinduzi  huo wamesema   wameomba   kufanyika  kwa  ziara  za  kupata  utaalamu  ikiwa  pamoja  na  wafanyabiashara  wa  nchini  india  kuja  Zanzibar  kwa  ajili  ya  kupeana  mbinu na uzoefu  wa kibiashara.

Mapema  Mh  Hassan alikagua  maonesho  ya  baadhi  ya  biashara  zinazoingia  hapa  nchini  kutoka  nchi  india ili  kuwa  ni fursa  moja  wapo  ya  kushirikiana  kibiashara  ili  nao   waweze  kupeleka  Nchini   India.

Powered by Live Score & Live Score App