Daily Archives: February 22, 2019

SERIKALI INAAZMA YA KUJENGA BARABARA MPYA KUTOKA CHAKECHAKE HADI MKOANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema serikali inaazma ya kujenga barabara mpya kutoka chakechake hadi mkoani, kutokana na umuhimu uliopo na kukidhi mahitaji ya wakati.

Dk. Shein amesema hayo wakati akifanya majumuisho ya ziara yake katika wilaya ya mkoani pemba, ambapo alipata fursa ya kuweka jiwe la msingi barabara ya mkanyageni – kangani pamoja na kufungua jengo la skuli ya michenzani na hatimae kupokea taarifa za kazi za serikali katika wilaya ya mkoani.

Akizungumza na wanachama na viongozi wa ccm pamoja na serikali ya wilaya ya mkoani, Dk. Shein alisema serikali inaendelea na hatua za kumpata mtaalamu ataefanya utafiti wa kina kujua barabara hiyo itakuwa ya aina gani na maeneo yepi itakapopita.

Alisema serikali pia inashughulikia suala la upatikanaji wa fedha za kuendesha mradi huo.

Dk.Shein alisema angependa kuona taarifa hizo anazipata mapema zaidi ili aweze kujua ni benki gani ya kuomba mkopo wa kuendeshea mradi huo.

“ni muhimu kuwa nabarabara nyengine kutokana na umuhimu wa wananchi, na taarifa itabainisha ‘design na gharama zake‘, alisema.

Katika hatua nyengine Dk. Shein alisema serikali inaendlea na juhudi za kutafuta vivuko vitakavyo kuwa na uwezo wa kuvusha wananchi kwa salama na amani katika maeneo ya visiwa vyote vidogo unguja na pemba.

MISRI YATARAJIA KUJENGA KIWANDA CHA KUZALISHIA UMEME HAPA NCHINI

Waziri wa kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi Mhe Rashid Ali Juma  amefanya mazungumzo na wawekezaji kutoka Misri ambao wanatarajia kujenga kiwanda cha  kuzalishia umeme kitakacho tumia  takataka  na  mabaki ya kilimo ambayo yatawezesha kuendeshea kiwanda hicho.

Akizungumza na wawekezaji hao ofisini kwake maruhubi walipokwenda kwa ajili ya kutambulisha miradi yao, ameeleza  kuwa  uwekezaji wa kiwanda cha umeme kitaleta manufaa makubwa kwa wananchi pia kuweza kufanya utafiti wa upatikanaji wa takataka katika  nchi ambazo zitatumika katika uzalishaji kwa manufaa ya wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Nae Naibu katibu mkuu Ahmad Kassim Juma amewaomba wananchi kutowa mashirikiano  kwa serekali  na wawekezaji  ili kuweza kusaidia jamii  kujikwamuwa na umasikini na kujipatia umeme unaozalishwa nchini.

Nae mwenyekiti wa wawekezaji  Nd. Mohamoud  Haroun ameushukru  uongozi wa Wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi kwa mashirikiano mazuri yatakayowezesha kufikia lengo la ujezi wa kiwanda hicho hapa nchini.

OFISI ZA SERIKALI NA TAASISI ZAKE KUTUMIA MFUMO MPYA WA UTUNZAJI WA NYARAKA

Waziri wa katiba sheria, utumishi wa umma na utawala bora Mhe Haroun Ali Suleiman ametoa wito  kwa ofisi za serikali na taasisi zake kutumia mfumo mpya wa utunzaji wa  nyaraka pamoja na mfumo wa kielectronic wa uhifadhi taarifa za watumishi wa umma.

Wito huo ameutoa wakati alipokuwa akitembelea sehemu za utunzaji wa nyaraka, mfumo wa uhifadhi taarifa na mfumo  udhibiti wa usalama katika jengo la ofisi ya rais katiba, sheria, utumishi wa umma na utawala bora.

Amewapongeza watendaji kwa kuweka mfumo wa kisasa wa boxwa utunzaji nyaraka unaozingatia vigezo vyote vya uhifadhi ambao ni mfumo wa kwanza zanzibar mradi uliotumia shilingi milioni 45, badala ya milioni 50 zilizokadiririwa.

Aidha mwalimu Haroun amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar imefanya  jitihada za makusudi za kuhakikisha kunakuwepo na kamera katika sehemu za barabaranilengo ni kuimarisha ulinzi, hivyo kutaka  majengo ya serikali yafungwe kamera katika kuimarisha usalama wa mali za serikali na kupambana na uhalifu.

Nae afisa tehama Nd.Khalid Mbarak Abdallah amesema  jumla ya kamera 12 awamu ya kwanza zimefungwa katika  ofisi ya rais katiba sheria utumishi wa umma na utawala bora  na mfumo wa kieletroni unafanya kazi vizuri kupitia serikali mtandao.

KUTOKUWEPO USHIRIKIANO KUNACHANGIA UFAULU MDOGO WA WANAFUNZI

Mkuu wa wilaya ya Magharib A kempeni Khatib Khamis Mwadini amesema ufaulu mdogo wa wanafunzi kwa skuli za wilaya hiyo unachangiwa na kutokuwepo ushirikiano baina ya wazazi na walimu.

Kauli hiyo ameitowa wakati akifungua mkutano wa walimu wakuu, kamati za skuli pamoja na wanafunzi wa skuli za wilaya hiyo wa kuimarisha mradi wa familia.

Amesema serikali inajitahidi kuzipatia nyenzo muhimu skuli zote ili wanafunzi waweze kufaulu vizuri katika masomo yao.

Nae mratibu wa mradi wa wanafunzi wa sos eveni baruti amesema lengo la mkutano huo ni  kuwawezesha wanafunzi kuepukana na matatizo katika  na waongeze juhudi katika masomo yao.

Nao washiriki katika mkutano huo wamesema ni vyema serikali kufanya utafiti na kuelimisha wazazi umuhmu wa elimu kwa kuwapunguzia kazi za nyumbani na kuwapa muda wa kudurusu masomo yao.

Powered by Live Score & Live Score App