Daily Archives: February 26, 2019

TAKRIBAN TANI 1.6 ZA BIDHAA MBALI MBALI ZA VYAKULA ZIMETEKETEZWA

Takriban tani 1.6 za bidhaa mbali mbali za vyakula ambazo hazifai kwa matumizi ya wanaadamu zimeteketezwa na bodi ya chakula na dawa zanzibar

akitoa ufafanuzi wa zoezi hilo kaimu mkurugenzi mtendaji wakala wa chakula na dawa Zanzibar Dr Khamis Ali Omar amesema bidhaa zote hizo zilizoteketezwa zimetoka katika makampuni mbali mbali nchini baada ya wamiliki wa kampuni hizo kuona bidhaa zao hazifai kwa matumizi ya binaadamu kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuishiwa na muda wa matumizi.

amesema bodi ya chakula na dawa inawataka wafanya biashara wanapoona bidhaa zao hazifai ni vyema wakatoa taarifa ili kuweza kufanyika taratibu za kuziteketeza bidhaa hizo kabla ya kuwafikia wananchi kwa ajili ya matumizi.

aidha ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za wafanya biashara wasio waaminifu katika uingizaji na uuzaji wa bidhaa zisizokubalika ili ziweze kuchukuliwa hatua za haraka kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa zenye usalama.

VIJANA NCHINI WATAKIWA KULINDA LUGHA YA KISWAHILI KWA MAENDELEO ENDELEVU.

Mkuu wa mkoa mjini magharibi Mhe Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka vijana nchini kulinda lugha ya kiswahili kwa maendeleo endelevu.

wito huo ameutoa katika maadhimisho ya lugha mama duniani ambapo Zanzibar imeungana na mataifa mengine duniani amesema vijana wana jukumu kubwa la kulinda lugha ya kiswahili kwa maendeleo ya taifa hivyo ni vyema kutumiwa vizuri na hakipotoshwi.

akisoma risala kwa niaba ya waandaji wa maadhimisho hayo mwenyekiti wa umoja wa mataifa chapter suleimani bakari amesema wao kama vijana wameamua kuadhimisha siku hiyo ili kulinda na kudumisha utamaduni wa mzanzibar.

nae mbunge wa viti maalum anaewaklisha asasi za kiraia bungeni khadija hassan aboud amewataka vijana hao kutumia lugha mama ya kiswahili katika kulinda utamaduni wa mzanzibar na mtanzania.

akizungumza katika ghafla hiyo balozi wa vijana katika maendeleo endelevu ambaye pia naibu katibu mkuu wa asasi ya vijana wa umoja wa mataifa vyuo vikuu ahmada salum suleimani amewashauri vijana kutumia lugha ya kiswahili katika kudumisha amani ya nchi.

maadhimisho ya lugha mama duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 21 mwezi wa pili ambapo zanzibar imeadhimisha siku hiyo tarehe 23 mwezi wa pili.

maadhimisho hayo yaliandaliwa na vijana wa chuo kikuu wanaodhaminiwa na umoja wa mataifa (un chapter).

 

WANA KIJIJI CHA CHARAWE WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MARADHI MBALI MBALI

Zaidi ya watu mia moja na hamsini wa wamefanyiwa uchunguzi wa maradhi mbali mbali na kupatiwa matibabu katika kijiji cha charawe ikiwa ni miongoni mwa kuadhimisha miaka arubaini na mbili ya kuzaliwa kwa ccm.

Akizungumza na zbc mara baada ya kumalizika zoezi hilo mwenyekiti wa group la wapenda maendeleo Zanzibar Hassani Abdallah Abasi amesema wameamua  kuisaidia jamii hasa vijijini katika sekta ya afya kwani ni marachache kufikiwa, pamoja na kuiunga mkono serikali katika juhudi za kuimarisha afya za wananchi wake

Sheha wa shehiya ya charawe Miraji Haji amesema wanakijiji hicho wasumbuliwa zaidi na maradhi ya macho, nyonga na presha na amewashukuru wananchi kuweza kujitokeza kwa wingi katika kupatiwa matibabu na kujuwa afya zao.

Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kusin unguja Latifa Khamis Juwakali amelishukuru umoja huo kwa kutowa huduma za afya katika maeneo ya vijijini  na ametowa wito kwa taasisi mbali mbali kusaidia jamii kusaidia huduma za afaya wananchi hasa maeneo hayo.

Powered by Live Score & Live Score App