Monthly Archives: February 2019

MAJAJI NA MAHAKIMU WANATAKIWA KUENDESHA KESI KWA HARAKA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mhe, Haroun Ali Suleiman amewataka Majaji na Mahakimu Kuendesha Kesi kwa Haraka ili Wananchi WawezeKupata haki zao katika kipindi  kifupi.

Amesema kufanya hivyo Itaonyesha Uwajibikaji wa Haraka katika Utekelezaji wao wa usimamizi waSheria katika kuwapatia haki kwa wananchi na hivyo wananchi kujenga imani na tasisi hiyo

Akifungua Maonesho yaMaadhimisho ya Sku ya Sheria huko Gombani Chake Chake, Mhe Haroun amewahimiza Wananchi kuyatumia Maonesho Hayo kwa kujifunza na kufahamu Taratibu Sahihi za kujua haki zao na jinsi ya kuzipata.

Amesema Fursa hiyo Iitumiwe na Majaji na Mahakimu  kuwashauri wananchi katika Kutatua Matatizo yao kwa kushirikia na sekta  ya Sheria ili kujuwa Njia za kuyatatua bila ya kuwepo kwa migogoro.

Aidha Mhe, Haroun Amekemea Vitendo vya Unyanyasaji Vinavyojitokeza kila siku hasa kwa Watoto na kuwahimiza Mahakimu kuangalia Sheria  na kuzitumia kwa Kuviangamiza Vitendo hivyo.

Akizungumzia Maonesho hayo Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu Amesema Maonesho hayo kufanyika Pemba ni Utekelezaji wa Agizo la Rais Dk. Shein kuitaka mahkama kuyafanya kisiwani humo ili wananchi wanufaike baada ya kufanyika kisiwani unguja takribani mara mbili.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdalla kwa Niaba ya Wananchi amesema maonesho kufanyika Gombani ni moja ya Mafanikio na Mashirikiano kati ya Tasisi za Umma na Jamii.

 

MASHUA YA PLASTIKI IMEIWEKA ZANZIBAR KATIKA RAMANI YA DUNIA

 

Ujio wa Mashua ya Mazingira Iliyotengenezwa kutokana na Malighafi ya Plastiki kutoka Nchini Kenya Chini ya Ushauri wa Taasisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa unaiweka Zanzibar katika Ramani ya Dunia kwenye Mapambano yake Dhidi ya Uchafuzi wa Mazingira.

Mashua hiyo ambayo tayari imeshaondoka jana kutoka mombasa nchini kenya inaingia Wete Kisiwani Pemba, kupitia Mkoani Pemba, Nungwi Mkoa Kaskazini Unguja na kutarajiwa kuingia  Forodhani Mjini Zanzibar mnamo tarehe 6 mwezi huu.

Kikao cha Washirika wanaosimamia na kushughulikia masuala ya Mazingira kutoka Taasisi za Umma, Binafsi pamoja na zile za Kimataifa  walikutana kujadili ujio wa Mashua hiyo chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdullah Hassan Mitawi kilichokutana Vuga Mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar Nd. Juma Mjaja aliwaelezea Wajumbe wa Kikao hicho kwamba lengo la Mashua hiyo ni kuihamasisha Jamii juu ya kuelekeza nguvu zao katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira yanayoleta Mabadiliko ya Tabia Nchi Duniani.

Nd. Mjaja alisema Tarehe 7 Febuari siku Moja baada ya kuwasili Mashua hiyo kutakuwa na uzinduzi wa usafi wa Mazingira katika Ufukwe wa Forodhani utakaoshirikisha Taasisi tofauti zinazojishughulisha na masuala ya Mazingira Zanzibar.

Naye kwa upande wake Ofisa wa Uratibu katika masuala ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bibi Clara Makenya alisema usafishaji wa Mazingira katika Pwani ya Forodhani itaongozwa na Muungano wa Taasisi za Kimazingira ya Les Do It Company Zanzibar.

NAIBU WAZIRI AKABIDHI VIFAA KWA KIKUNDI CHA TAIFA CHA TAARAB

Naibu Waziri wa Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo Lulu Msham Abdalla amesema Wizara yake itahakikisha kikundi cha Taifa cha Taarab kinafanya kazi zake vizuri ili kuendelea kukuza sanaa ya Muziki wa Tarab Visiwani hapa.

Amesema asilimia kubwa ya wananchi wa Zanzibar katika mkiaka ya zamani walikuwa ni wapenzi wa muziki wa Tarab Asilia kama ilivyokuwa wakazi wa Tanga na Mombasa na kwamba Serikali inataka hali hiyo iendelee kuwa hivyo

Naibu waziri huyo ameyasema hayo wakati akikikabidhio kikundi cha Taifa cha Taarabu  na kusema wiraza yake imekitayarishia bajeti kikundi hicho kiliochosheheni waimbaji machachrii na wacharaza alla makini.

Amesema katika kuhakikisha kikindi hicho kinaimarika zaidi kitashirikishwa katika matamasha mbali mbali ya muziki ndani na nje ya nchi.katibu wa kikundi hicho pamoja na msanii Profesa Moh’d Iliyas wametowa shukrani kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuweza kuwajali wasanii wa hapa nchini.

Mshauri wa Rais Sanaa na Utamaduni Chimbeni Kheri amesema wasanii wa kikundi cha taifa wanatoka katika vikundi mbali mbali hapa Zanzibar hivyo amewataka kuzidisha umoja na mashirikiano katika uwendeleza muziki wa taarab asili.

Naibu Katibu wa Wizara ya Vijana Sanaa,Utamaduni na Michezo Amour Hamil ameseama katika bajeti ya mwaka 2019/2020 watahakikisha wizara kukiendeleza zaidi kikundi hicho kwa kukipatia vyombo vya muziki .

BALOZI SEIF ALI IDDI KUUAGIZA UONGOZI WA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR KUWASIMAMIA WATENDAJI WAO

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameendelea kuuagiza uongozi wa wizara ya afya zanzibar kuwasimamia watendaji wao kufanyakazi katika Hospitali na Vituo vya Afya vilivyopo Kisiwani Pemba.

Amesema wakati umefika kwa Viongozi wa Wizara hiyo kuacha tabia ya kuwabeba Wafanyakazi wanaotaka uhamisho wakati uajiri wao wa kazi kwa mujibu wa Mikataba yao na Sheria za Utumishi wa Umma uko Kisiwani pemba.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar ulioongozwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Harus Said Suleiman ulipofika kumpa Taarifa ya masuala mbali mbali yaliyochukuliwa hatua katika vitengo vya Wizara hiyo.

Alisema haipendezi kuona baadhi ya Watendaji wamesomeshwa na Serikali kwa gharama kubwa kwa lengo la kuwahudumia Wananchi lakini badala yake huamua kuchagua maeneo ya Kufanya kazi jambo ambalo Serikali Kuu haitakuwa tayari kuona linaendelezwa.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameupongeza Uongozi wa Wizara ya Afya pamoja na Wafanyakazi wake kwa jitihada kubwa unazochukuwa za kukabiliana na changamoto zinazowakabili ambazo wakati mwengine huleta usumbufu kwa Jamii.

Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bibi Asha Ali Abdulla alisema Uongozi wa Wizara hiyo umejianza kujiwekeza utaratibu wa kujenga Utamaduni wa kutoa Taarifa ya mambo mbali mbali yanayotekelezwa na Wizara hiyo ili jamii ielewe kinachofanyika kila hatua.

Bibi Asha alisema mfumo uliopo hivi sasa wa kusubiri kuripoti matatizo yanapotokezea hautoi nafasi nzuri kwa Serikali kujipanga vyema katika kukabiliana na changamoto kubwa zinazojichomoza kwenye Taasisi zake.

Alisema yapo masuala yaliyoanza kuchukuliwa  hatua na Uongozi wa Wizara katika azma ya kuondoa kero na hitilafu zinazoleta usumbufu kwa Uongozi wenyewe, Wafanyakazi sambamba na Wananchi wanaohitaji huduma kupitia Taasisi hiyo ya Kiafya.

Bibi Asha alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba matumaini ya ujenzi wa Nyumba za Wafanyakazi wa Hospitali ya Abdullah Mzee Mkoani yameanza kutoa matumaini kutokana na China kuonyesha nia ya kutaka kufadhili Mradi huo.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya alisema ipo miradi mengine ambayo kwa wakati huu iko katika hatua za utekelezaji akatolea mfano matengenezo ya Lifti ya Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja yalaiyokuwa katika hatua za mwisho yakienda sambamba na ununuzi wa Lifti nyengine Mpya ya Hospitali hiyo.

Alisema hakati za maandalizi ya Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa hapo Kikungwi zimeanza baada ya kukamilika kwa uchambuzi yakinifu wa eneo lote la mipaka, ujenzi wa Ghala ya kuhifadhia Dawa huko Vitongozji Kisiwani Pemba, Ujenzi wa jengo jipya la Hospitali ya Wagonjwa wa akili pamoja na kukamilika kwa Kitengo cha uchunguzi wa Vinasaba.

 

 

 

Powered by Live Score & Live Score App