Daily Archives: March 1, 2019

TIMU YA JIMBO LA WETE IMEFANIKIWA KUTWAA UBINGWA WA MASHINDANO YA MAIDA CUP.

Timu ya jimbo la Wete imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindandano ya Maida Cupya kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwakwa CCM, baada ya kuitandika timu ya jimbo la Micheweni bao 2-1.

Mchezo huo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa Konde Polisi, Jimbo la Wete iliyovalia jazi ya nja nailikuwa ya kwanza kulionalango la wapinzani wake kupitia kwa mchezaji Ali Mohamed kufunga mabao hayo katika dakika ya 22 na 49, huku Micheweni ikasawazishwa kupitia kwa Abdalla Khatib dakika ya 43.

Akizungunza na wanamichezo na washabiki, Mwenyekitiwa CCM Mkoawa Kaskazini Pemba, Mberwa Hamad Mberwa, amempongeza Mbunge  Maida kwa kuwaunga mkono vijana kupitia sekta ya michezo.

Mdhamini wa mashindano hayo na Mbunge wa kuteuliwa wa UWT Maida Hamad Abdalla, amesema mashindano hayo yamekusudia kutafuta vipaji vya wachezaji watakaounda timu ya Wilaya ya Wete na Mkoa.

Kwa  upande wa wanamichezo hao wamesem mashindano hayo yameamshaari katika timu zao.

Timu Wete imekabidhiwa shilingi laki mbili, kikombe, seti mbili za jezi, nishani na mipira mitatu, mshindiwa pili Micheweni ikipatiwa shilingi laki moja, jezi seti moja, mipira miwili na midali ya silva.

Huku zawadi mbalimbali zikitolewa ikiwemo kipa bora, mchezaji bora, mchezaji mwenye nidhamu, pamoja na timushiriki kila mmoja ikipatiwa mpira mmoja mmoja.

WANANCHI PUJINI WAMAETAKIWA KUTOA MASHIRIKIANO WAKATI WA UJENZI WA NGOME YA MKAMANDUME

Mkuu wa Wilaya ya ChakeChake Rashid Hadid Rashid amewataka wananchi wa Pujini wilaya ya Mkoani kutowa ushirikiano wakati wa ujenzi wa Ngome ya Mkamandume ili kufanikisha malengo ya serikali ya kurudisha haiba ya eneohilo.

Nd. Rashid ametowa wito huo kwenye mkutano wakukabidhi eneo la Mkamandume kwa Mkandarasi atakaejenga ngome hiyo Nd. Mansour Mohamed Kassim kutoka kampuni ya SHAMJO LTD.

Amesemaserikaliimekusudiakuliimarishaeneohilokwakurudishahistoriayakekubwaambayoinawavutiawagenikutokanchimbalimbaliduniani.

Akitowa maelezo ya eneo hilo Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Salum Kitwana Sururu na Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Khatib Juma Mjaja wamewasisitiza wananchi wa eneo hilo kudhibiti uharibifu na wizi katika kazihiyo.

Kwa upande wake Mkandari wa mradi wa ujenzi wa Ngome yaMkamandume Mansour Mohamed amesema watafanyakazi hiyo kwa kiwango kinachotakiwa na watawashirikisha wananchi katika harakati za ujenzi ili waanze kufaidika na Ngomehiyo.

Mradi wa ujenzi wa Ngome ya Mkamandume unakwenda sambamba na ujenzi wa gofu la Fukuchani Unguja ambayo kwa pamoja itagharimu kiasi cha shilingi milionimia 800.

UHUSIANO WA KARIBU BAINA YA OMAN NA ZANZIBAR UNAZIDI KUKUA.

Uhusiano wa karibu baina ya Wizara ya Habari, Utalii na mambo ya Kale Zanzibar na mamlaka ya Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa ya Oman unaendelea kukua kila wakati kufuatia ukaribu uliopo wa viongozi wa kitaifa wa Oman na Zanzibar.

Mwenyekiti wa mamlaka ya Nyaraka na Makumbusho ya Kitaifa wa Oman Dr. Hamad Mohamed  Al – dhawyany ametoa kauli hiyo akiuongoza ujumbe wa viongozi 12 wa taasisi hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi vuga Mjini Zanzibar.

Dr. Hamad Mohamed  Al – dhawyany alisema Historia ya kidamu muda mrefu iliyopo kati ya wananchi wa Zanzibar na Oman inazidi kuongeza ushawishi wa ushirikiano katikanyanja tofauti zinazozidi kuongezeka siku hadi siku.

Alisema uimarishaji wa jumba la ajabu Forodhani, pamoja na magofu ya kihistoria yaliyopo Mtoni chini ya ufadhili wa Oman utakapokamilika utatoa fursa kwa wageni na watalii kutembelea kitendo ambacho mbali ya kuimarisha historia hiyo muhimu lakini pia kitaongeza mapato ya taifa.

Dr. Hamad Mohamed  Al – dhawyany alisema wakati matengenezo ya Jumba la Ajabu Forodhani yakiendelea pamoja, magofu ya kihistoria yaliyopo mtoni ujenzi wake unaweza kuanza wakati wowote kuanzia sasa kwa vite taratibu zote zimeshakamilika.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar inathamini sana ushirikiano wake na Oman kutokana na Historia ya wananchi wake walioingiliana kidamu.

Balozi Seif aliendelea kuipongeza Serikali ya Oman chini ya kiongozi wake Mahiri Mfalme Qaboos Bin Said kwa jitihada inazochukuwa za kuiunga mkono Zanzibar katika harakati zake za kujiletea maendeleo yaliyolenga kustawisha maisha ya wananchi wake.

Alisema ujio wa meli ya kifalme ya Oman katika visiwa vya Zanzibar miaka miwili iliyopita mbali ya wananchi wa Zanzibar  kufurahia ujio huo lakini pia imeleta baraka kubwa kutokana na mambo makubwa yaliyozaliwa kutokana na ziara ya meli hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba matengenezo ya jumba la ajabu forodhani, pamoja na magofu ya kihistoria ya mtoni ni miongoni mwa mambo yaliyozaliwa kutokana na ziara ya meli hiyo.

Balozi Seif alieleza kwamba majengo hayo yana heshima kubwa duniani kutokana na historia yake inayothaminiwa pia na shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni {unesco}  na kupelekea mji mkongwe za Zanzibar uliobeba majengo hayo kuingizwa katika urithi wa kimataifa.

Mapema waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo alisema hii ni mara ya pili kwa ujumbe wa mamlaka hiyo kutembelea Zanzibar kufuatilia maendeleo ya mikataba mbali mbali iliyotiwa saini kati ya Serikali za Oman na Zanzibar.

Mh. Mahmoud alisema yapo mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi ya pamoja ya pande hizo mbili akitaja kuwa ni pamoja na matangenezo ya beit al ajaib Forodhani, pamoja na majengo ya kihistoria ya Mtoni.

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI IMEPONGEZWA KWA KUFANYA KAZI ZAKE VYEMA

Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki imepongezwa kwa kufanya kazi zake vyema katika kipindi cha miaka 55 yaMapinduzi ya Zanzibar, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano na ushirikiano ndani na Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  alitoa pongezi hizo wakati alipofanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Damas Daniel Ndumbaro aliyefika ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo pamoja na kujitambulisha kwa Rais.

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alieleza kuwa licha ya kubadilishwa jina la wizara hiyo mara kwa mara lakini bado imekuwa ikifanya kazi zake vyema na kuonesha ushirikiano mzuri wa pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hata Nje ya Tanzania.

Hivyo, rais dk. Shein alisisitiza haja ya kuendeleza uhusiano na mashirikiano hayo mema na idara yake iliopo hapa zanzibar ili mafanikio zaidi yaweze kupatikana kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa ikizingatiwa kuwa wizara hiyo ni ya Muungano.

Rais dk. Shein alisema kuwa wizara hiyo ina historia nzuri na tayari imejijengea heshima  na sifa kubwa ndani na nje ya Tanzania, hivyo kuna haja ya kuiimarisha kwa lengo la  kupata mafanikio zaidi.

Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumpongeza Naibu Waziri wa Wizara hiyo kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kuweza kuukubali uteuzi wake huo ambao utamuwezesha kutekeleza vyema majukumu aliyopewa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Dk. Shein aliongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar itaendelea kuiunga mkono na kuipa ushirikiano wa aina zote Wizara hiyo kama ilivyo kwa wizara nyengine zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza matumaini yake makubwa aliyonayo kutokana na uongozi na utendaji kazi wa Naibu Waziri huyo katika wizara hiyo ambayo ni kubwa kutokana na umuhimu wake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nje ya Tanzania.

Nae Naibu Waziri wa Wizara ya mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Damas Ndumbaro alieleza kuwa wizara hiyo ina umuhimu mkubwa sana katika kuimarisha muungano uliopo sambamba na kuimarisha masuala  yote ya kiitifaki.

Aidha, Naaibu waziri huyo nae alieleza matumaini yake makubwa kutokana na utumishi uliotukuka wa Rais Dk. Shein katika uongozi wake hali itakayompelekea kufanya kazi zake vyema na kuweza kutekeleza lengo lililokusudiwa kwa mafanikio ya pande zote mbili za jamhuri ya muungano wa tanzania.

Sambamba na hayo, Naibu Waziri huyo alimueleza Dk. Shein kuwa wizara ya mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wanaridhika na utendaji mkubwa wa kazi anazozifanya Dk. Shein katika kuwatumikia wananchi wa Zanzibar na Tanzania nzima kwa jumla na kutumia fursa hiyo kumpongeza kwa juhudi zake hizo

Hivyo, naibu waziri huyo alimuhakikishia Rais Dk. Shein kuwa amepokea maelekezo na ushauri aliopewa na rais na kumuahidi kuwa atayafanyia kazi mambo yote huku akisisitiza kuwa kipindi kirefu atajitadi kufanya kazi zake hapa Zanzibar kwa azma ya kustawisha wizara hiyo kupitia idara yake ya uratibu ya hapa Zanzibar.

Dk. Damas  Daniel ndumbaro ambaye ni mbunge wa Songea mjini katika mkoa wa Ruvuma aliteuliwa kushika wadhifa huo Septemba 26 mwaka jana 2018 akichukua nafasi ya Dk. Suzan Alphonce kolimba ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. JohnJoseph Magufuli.

Powered by Live Score & Live Score App