Daily Archives: March 1, 2019

ASSASI ZA KIRAIYA ZAWASAIDIA VIJANA JUU YA SUALA ZIMA LA KUJIKWAMUA NA UMASIKINI

Imeelezzwa  kwamba   assasi za kiraiya  zimekuwa kionyesha mchango mkubwa katika kuwasaidia  vijana  juu ya suala zima la  kujkwamua na umasikini na  kuwachana na  utegezi .

Hayo yameelezwa na washiriki wa kongamano  la siku mbili  lililoandaliwa na  mwamvuli wa asassi  za kiraiya  Zanzibar  angoza  huko katika hoteli  ya Zanzibar beach mazini mjini  nguja.

Wamesema  kongamano hilo lililojasdili  mada  mbali mbali  limewaibua mbinu  za namna ya kujua  haki zao  kwa jumuiya  wanazo zianzisha  ikiwemo la taratibu za kujisajili wakatim wanao ajista jumuiya  ama taasisi.

Mwenyekiti wa  mwamvuli wa asasi za kiraiya ZanZibar angoza  Bi Asha Aboud amesema kongamano hilo litaondoka nam na maazimio ambayo yataibua hisia ya  kuweza kujipanga zaid katika utendaji wa kazi kwenye miaka ijao.

Akifunga kongamano hilo katibu mkuu wa shirikishom la vyama  vya wafanyakazi Zanzibar Nd  Khamis Mwinyim Mohammed  amewataak viongozi wa mwamvuli wa asasi za kiraiya  zaznibar angizo kufnya kazi  kwa kujenga demokrasia  na utawala bora.

Kongamano hilo la siku mbili  limewashirikisha watu kutoka katika  jumuiya na taasisi mbali mbali kutoka Unguja, Pemba  na Daarisalamu.

NBS YAFANYA MAPITIO YA KANUNI ZA TAKWIMU ZA MWAKA 2017

Ofisi ya Taifa ya takwimu (NBS) inafanya mapitio ya kanuni za takwimu za mwaka 2017 ili kuwezesha marekebisho ya sheria ya takwimu no 9 ya mwaka 2015 kwa lengo la kuimarisha mfumo wa uzalishaji  na utoaji wa takwimu na sio kudhibiti uzalishaji takwimu.

Mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu Dr. Albina Chuwa ameeleeza hayo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya marekebisho ya sheria hiyo  ambayo ilitungwa mwaka 2015 na kurekebishwa kupitia sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali na: 8 ya mwaka 2018.

Dr. Albina ameyabainisha maudhui makuu manne yaliyojikita kwenye  marekebisho ya sheria iliyopo kuwa ni  pamoja na kuweka  utaratibu wa uchambuzi wa kina kwa kutumia kanzi data ambazo zimeshatolewa na nbs, kuainisha mwongozo wa utoaji wa takwimu ambazo zinatofautiana na zilizotolewa na nbs, kuzuia utoaji wa takwimu zenye nia ya upotoshaji, na kuweka utaratibu wa uchapishaji wa taarifa za kitakwimu.

Aidha Dkt Albina amefafanua  kuwa marekebisho hayo ya sheria, yatachanganua na kuainisha namna bora ya utekelezaji wa matakwa ya sheria.

Kw aupande wake mkurugenzi mtendaji  wa taasisi ya utafiti ya repoa Dr. Donald Mmari amesema miongozo katika sheria inaelekeza wanatakwimu kutumia njia sahihi ili kupata takwimu bora.

WANANCHI WAKUBALI KUVUNJA NYUMBA ZAO KATIKA ENEO LINALOTARAJIWA KUJENGWA BARABARA

Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amewapongeza wananchi wa shehia za Kinuni, Mwembemajogoo na Nyarugusu kwa kukubali kuvunja nyumba zao katika eneo linalotarajiwa kujengwa barabara ya Tundaua – Kinuni Skuli kuanzia mwezi ujao.

Akizungumza na wananchi wa maeneo hayo jana baada ya kukagua eneo la ujenzi wa barabara hiyo, amesema hatua hiyo ya kizalendo inahitaji pongezi kwani inaunga mkono juhudi za serikali ya Zanzibar ya  kuwafikishia maendeleo wananchi wake.

Alisema uamuzi wa kujenga barabara hiyo unatokana na agizo la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alilolitoa wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa skuli 9 za kisasa za Unguja na Pemba katika shehia ya Kinuni, wilaya ya Magharibi ‘B’, Unguja mwezi Januari mwaka huu ili kurahisisha mawasiliano kati ya wananchi wa eneo hilo na maeneo mengine ya mkoa huo.

Aidha Mkuu wa Mkoa amesema ujenzi huo pia umezingatia umuhimu wa barabara hiyo kiuchumi na kijamii utaiunganisha barabara hiyo na barabara ya Magogoni - Tundaua – Kijitoupele iliyojengwa mwaka 2016/2017, utapunguza changamoto ya usafiri inayowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Mheshimiwa Ayoub aliyeambatana na viongozi, maafisa na watendaji mbali mbali wa ngazi ya Mkoa,Wilaya,Manispaa,Wizara na viongozi wa Jimbo la Pangawe katika ziara hiyo iliyolenga kukagua maandalizi ya ujenzi huo, aliwahakikishia wananchi hao kuwa serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na Manispaa ya Magharibi ‘B’ itatoa matofali 2,000 na mifuko 100 ya saruji itakayogaiwa kwa wananchi walioathiriwa na ujenzi huo ili kuharakisha marekebisho ya nyumba zao kupisha ujenzi huo.

Ili kufikia mustakabali mzuri wa ugawaji wa msaada huo Mhe Ayoub aliagiza kuundwa kwa kamati maalum inayotokana na wananchi wenyewe itakayofanya kazi kwa karibu na masheha wa shehia maeneo hayo ili kuratibu ugawaji wa msaada huo na kuongeza muda wa kuondoa majengo hayo hadi machi 15 mwaka huu badala ya machi 1.

Awali wakizungumza katika ziara hiyo baadhi ya wananchi wa maeneo yaliyoathiriwa na ujenzi wa barabara hiyo wamesema wameupokea kwa mikono miwili ujenzi huo na kuomba kupatiwa fidia kutokana na athari walizopata na kuongezewa muda uliowekwa kuondoa majengo yao.

Akitoa maelezo katika hafla hiyo Mhandisi Mkuu wa wizara ya nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa, serikali za mitaa na idara maalum za SMZ Ali Omar Ali alisema barabara hiyo itakayojengwa kwa kiwango cha lami itakuwa na urefu wa kilomita 1 na upana wa mita 7 unaojumuisha mita 6 za lami na mita 1 ya mabega ya barabara itakayotumika kwa mitaro ya maji ya mvua.

Amesema usanifu wa barabara umefanyika kwa umakini mkubwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha barabara inajengewa njia maalum za kupitishia maji ya mvua ili iwe imara zaidi lakini pia maji hayo yasiathiri makaazi ya wananchi.

Ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kuchukua muda wa miezi 6 hadi kukamilika kwake, unajengwa kwa fedha za serikali ni mwendelezo wa uimarishaji wa miundombinu ya barabara za ndani katika Mkoa wa Mjini Magharibi unaofanywa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na ahadi na maelekezo ya viongozi wakuu wa serikali.

Powered by Live Score & Live Score App