Daily Archives: March 6, 2019

MFUMKO WA BEI KWA MWEZI FEBUARI UMESHUKA KWA ASILIMIA MBILI

Ofisi ya mtakwimu mkuu wa serikali kupitia kitengo cha takwimu za bei kimeeleza kuwa mfumko wa bei kwa mwezi febuari umeshuka  kwa  asilimia  mbili nukta sita ukilinganisha na asilimia  tatu nukta sifuri ya mwezi wa januari 2019.

Akitoa taarifa  kwa  waandishi wa habari mkuu wa kitengo cha takwimu  za bei ndugu khamis abdul rahaman msham amesema  mfumko wa bei wa  bidhaa zisizokuwa za chakula umeshuka  kwa asilimia moja nukta saba  katika  mwezi wa febuari 2019  ukilinganisha na asilimia mbili nukta nne kwa mwezi uliopita.

Akitolea ufafanuzi zaidi mhadhiri mkuu idara ya uchumi wa chuo kikuu cha taifa suza dr suleiman simai msaraka amesema kasi ya kupanda kwa bei ndio iliyoshuka kwa mwezi huu wa febuari ukilinganisha na nchi za afrika mashariki.

wakati huo huo mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati zanzibar zura imesema kupungua kwa nishati ya mafuta takriban siku mbili wiki hii kumetokana na zoezi la kuteremsha nishati ya mafuta katika meli  ya mafuta.

Ufafanuzi huo umetolewa na afisa mwandamizi wa zura ndugu omar Ali Yussuf.

 

WANANCHI WAMEIOMBA SERIKALI KUYAFANYIAKAZI HARAKA MIUNDOMBINU YA PITAYO MAJI

Wananchi    wameiomba  serikali  kuyafanyiakazi  haraka  miundombinu  ya  pitayo  maji  mvua   ili  kuweza  kuwanusuru  wakaazi wa  maeneo  ya  mabondeni  na  mvua  za  masika  zinazotajiwa  kunyesha  hivi  karibuni.

Wakizungumza  na  zbc  wakaazi  wa  maeneo  ya  bububu  ,  mpendae  kwabiti  hamrani  wamesema  wanaishukuru  serikali  kwa  maandalizi  ya  ujenzi  wa  mitaro  mikubwa  ipitayo  maji  kwani  kufanya  hivyo  kunawezesha  kutatua  changamoto  hiyo   kwa kila  nyakati  za  mvua  zinapowadia.

Wamesema   kuitekeleza  amri  ya  serikali  kuhama  maeneo  hayo  inawawia  vigumu  kutokana na  ukosefu  wa  makaazi  hivyo  wameiomba  serikali  kuiharakisha  miundombinu  iweze  kukidhi  kina  kikubwa  cha  maji  ili  kuweza  kubaki  maeneo  yao  pasi  na  uharibifu  wowote  kutokea katika  maeneo  yao.

Imekuwa  ni  utaratibu   kwa  wananchi kupewa  hifadhi  ya  makaazi  kwa  kila  msimu  wa  mvua  za  masika  zinapowadia  kutokana na  athari  zinazowapata  wakaazi  wa  maeneo  ya  mabondeni  kwa  kukabiliwa  na  maafa  tofauti  ikiwemo  uharibifu  wa  mali  na  vifo  kwa  watoto kutokana  na  kuingiliwa na mali katika  makaazi  yao.

 

KUFUNGWA MKANDA KUTAONGEZA FURSA KWA WAGENI KUJA NCHINI.

Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya viwanja vya ndege zanzibar kamishana mtaafu hamdan omar amesema kufungwa kwa mkanda wa kubebea mizigo katika kiwanja cha ngege cha kimataifa cha abeid amani karume kutaongeza fursa kwa wageni kuja nchini.

Hamdan ameyasema hayo alipotembelea kiwanja hicho kuona hali inavyoendelea matumizi ya mkanda huo amesema mkanda huo umeleta ufanisi na kuongeza pato la taifa kutokana na wageni wanaoingia nchini.

Aidha amesema matarajio yao ni  kuwa mkanda huo utatumika kama ilivyokusudiwa na kuishauri mamlaka kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kiwanja hicho  ili kuweza kukabiliana na mabadiliko hayo.

Mkuu wa kitengo cha ict mohamed abdul khan  msoma amesema timu yake ikishirikiana na mtaalam kutoka nje ilitoa ushirikiano mzur ili kuhakikisha zoezi hilo linakwenda kama ilivyokusudiwa

Powered by Live Score & Live Score App