Daily Archives: March 7, 2019

MAMLAKA INATOA KIWANGO CHA KIMATAIFA KATIKA KUTOA HUDUMA ZILIZOBORA

Naibu waziri wa wizara ya ujenzi mawasiliano na Usafirishaji Mh Mohamed Ahmada amesema atahakikisha mamlaka inatoa kiwango cha kimataifa katika kutoa huduma zilizobora na kuwataka watendaji kufanya kazi kwa nidham na ushirikiano.

Akizungumza mara baada ya ya kutembelea katika kiwanja cha kimataifa cha Abeid Amani Karume amesema  serikali imepiga hatua kubwa ya kuwafikishia maendeleo wananchi wake.

Amesema nidham katika sehemu za kazi ndio inayo pelekea  kuipatia sifa  Zanzibar.

Hivyo amewaomba wafanyakazi wa kiwanja cha ndege kuzidisha ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao kwa  vile kiwanja kinatumiwa na wageni na watu wa aina mbali mbali.

Mkurugenzi mipango na miradi mamlaka ya viwanja vya ndege Seif Abdalla Juma ameitaja miradi inayo ambayo inatekeleza shughuli mbali mbali kiwanjani hapo.

Mkuu wa kitengo cha ict Mohamed Abdul Ghani Msoma  amezitaja baadhi ya changamoto ni pamoja na kutoelewa matumizi sahihi ya mkanda wa kupokea na kutoa mabegi

UTENDAJI KAZI UNAOZINGATIA MAADILI YA UWAJIBIKAJI UTAIWEZESHA WIZARA KUFIKIA MALENGO STAHIKI

Naibu waziri wa wizara ya elimu na mafunzo ya amali Mh. Simai Mohamed Said, amesema utendaji kazi unaozingatia maadili ya uwajibikaji pamoja na ushirikiano utaiwezesha wizara hiyo kufikia malengo yake iliyojipangia.

Mara baada ya kukabidhiwa ofisi na Mh Mmanga Mjengo Mjawiri ambae sasa ni waziri wa kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi, Mh Simai amewataka watendaji wakuu wa wizara ya elimu kutoa taarifa zenye usahihi ambazo zitafanikisha uwasilishaji bora wa utekelezaji katika vikao vya bajeti ya serikali.

Katika hafala hiyo waziri wa kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi mh mmanga mjengo mjawiri, amewataka watendaji wa wizara ya elimu kumpa ushirikiano naibu waziri huyo, ili kuwepa kuimarisha sekta ya elimu hapa nchini

SMZ YAPANGA MIPANGO MADHUBUTI YA KUHAKIKISHA INATOA ELIMU YA KUKABILIANA NA UKIMWI

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imepanga mipango madhubuti ya kuhakikisha inatoa elimu kwa watendaji juu ya kukabiliana na maambukizi mapya ya maradhi ukimwi.

Naibu Waziri wa Nchi afisi ya makamu wa pili wa Rais Mh Mihayo Juma Nunga ameeleza hayo alipofungua mafunzo kwa wafanyakazi wa ofisi hiyo katika ukumbi wa Shekh Idriss Abdulwakil kikwajuni

amesema ingawa maambukizi hayo yameshuka kwa Zanzibar lakini ni vyema kuchukua juhudi za kufikia tisini tatu ambayo ndio malengo ya dunia.

akitoa malengo ya mafunzo hayo mkurugenzi utumishi ofisi ya makamu wa pili wa Rais Bi Halima Ramadhan Taufik amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa watendaji wao ili kuwakumbusha athari za ugonjwa huo kwa watendaji na taifa.

akiwasilisha mada ya elimu ya msingi juu vvu na ukimwi na hali halisi ya ukimwi Zanzibar mkurugenzi mtendaji tume ya ukimwi Zanzibar amesema mafanikio juu ya mapambano ni vyema kwa taasisi kushirikiana pamoja na kuacha unyanyapaa

Powered by Live Score & Live Score App