Daily Archives: March 7, 2019

JAMII KUTOYAFUMBIA MACHO MASUALA YA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA ILI KUINUSURU JAMII

Naibu Waziri wa kazi uwezeshaji wazeee wanawake na watoto Mhe Shadya Moh’d Suleiman  amesisitiza  jamii  kutoyafumbia macho  masuala ya udhalilishaji  wa kijinsia   ili kuinusuru jamii.

Akifungua  kongamano  katika  shamrashamra  ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani  liloshirikisha  wanawake  kutoka  mikoa  yote  ya unguja  huko kwenye  ukumbi wa uwanja wa  watoto  kariakoo  amesema  tatizo  hilo si  la wizara peke yake na linamuhusu kila mmoja katika  nafasi yake.

Amesema tayari  mikakati  mbalimbali  imekuwepo  katika  kupambana na vitendo vya udhalilishaji  kijinsia ,   lililobaki  ni kufanyakazi kwa mashirikiano.

Mada mbalimbali   zimetolewa  katika  kongamano  hilo ikiwemo usafirishaji  haramu  wa binadamu ,   na ukatili  wa kijinsia  kwa wanawake  na watoto, ambazo  zimewasilishwa  na enna  lutengano  kutoka shirika la  kimataifa  uhamiaji,  na mohd  jabir  kutoka  idara ya wanawake na watoto.

Kongamano  hilo  lilopewa  jina,  kufikia  usawa wa kijinsia kwa  maendeleo  endelevu limetayarishwa  kati  ya wizara kuwww na shirika la kimataifa  la  wahamiaji (international organisation for  migration ).

Kauli mbiu ya siku ya wanawake   duniani  ni  kuwa  mbunifu, mahiri ,na  zingatia usawa katika ku leta mabadiliko kwa wote.

Powered by Live Score & Live Score App