Daily Archives: March 21, 2019

TASAF KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA WALENGWA WA KUNUSURU KAYA MASKINI KATIKA KUENDESHA MIRADI YAO

Kamati ya kusimamia viongozi wakuu wa kitaifa wa baraza la wawakilishi wamewashauri viongozi wa tasaf kuendelea kutoa elimu kwa walengwa wa kunusuru kaya maskini katika kuendesha  miradi yao ili kuweza kuingiza kipato zaidi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh  Panya Ali Abdalla  amesema hatua hiyo itaweza  kuwasaidia walengwa  kufanya kazi  zao kwa uhakika.

Akitoa ufafanuzi juu ya msimamo wa serekali  naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mhe Mihayo Juma Nunga amesema ni vyema kuhakikisha  kuwa hakuna mwananchi atakaeachwa  katika mpango  huo kwa awamu itakayofuata ili lengo la serikali la kuwasaidia wananchi liweze kufikiwa.

Mratib wa tasaf unguja  ndugu  Makame Ali  Haji  ameifahamisha kamati hiyo kwamba  miradi  ya mfuko wa maendeleo ya jamii tasaf  imeweza kusaidia vizuri wananchi  kwa kuongeza vikundi  vya ushrika kutoka 970  hadi 1151.

Walengwa  wa kunusuru kaya maskini wamesema  tasaf imeweza kuwasaidia sana katika  kuinua vipato  vyao  vya maisha .

Kamati hiyo  ilitembelea mradi  wa kubanja kokoto bungi ,mradi wa upandaji wa miti ya mikoko na wa mivinje kitogani,na shamba darasa l a migomba muyuni c

WANANCHI PAMOJA NA WANAFUNZI WAPEWA ELIMU JUU YA KUHAMASISHA ULIPAJI WA KODI KWA HIARI

Bodi ya mapato zanzibar imesema itaendelea kuelimisha wananchi pamoja na wanafunzi juu ya kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari ili nchi iongeze mapato kwa maendeleo ya wananchi wake.

Afisa elimu kutoka bodi ya mapato Bi Raya Suleiman ameyasema hayo wakati akizungumza na walimu na wanafunzi wa skuli za sekondari za fujoni na mfenesini  amesema  zanzibar imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za ukusanyaji wa mapoto hivyo ni vyema kujua umuhimu la kulipa kodi ili kuweza kutoa huduma bora za kijamii.

Nae afisa uhusiano kutoka zrb Bi  Badria Atai Masudi amesema wanafunzi wanawajibu wa kujua umuhimu wa kulipa kodi  na kupewa risiti wanaponunua bidhaa ili kuepuka matatizo yatakayoweza kujitokeza  baadae.

Nao walimu wamesema kuna mgongano wa ulipaji kodi kati ya tra na zbr hivyo wameomba waelimishwe juu ya ulipaji wa kodi huo.

 

Powered by Live Score & Live Score App