A ALHAJJ VUAI MWINYI MOHAMED AMEWATA WAISLAMU KUJITOKEZA KATIKA UZINDUZI WA JENGO LA MARKAZ IJTIMAI

 

 

Mkuu wa mkoa kaskazini unguja Alhajj Vuai Mwinyi Mohamed amewata waislamu kutoka katika maeneo mbali mbali ya zanzibar na tanzania kujitokeza katika uzinduzi wa jengo la markaz ijtimai kidoti unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu mkoa wa kaskazini unguja.

uzinduzi huo unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi na waislamu kutoka sehemu mbali mbali za tanzania ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mufti wa tanzania sheikh abubakar zubeir kwa ajili ya kuzindua jengo hilo  ambalo ujenzi wake unaendelea.

alhaj vuai amewaomba wananchi na wadau wengine kujitokeza ili kufanikisha shughuli hiyo muhimu huku akiwasisitiza  kuendelea kutoa michango yao ya hali na mali ikiwemo saruji ,nondo, matofali kwa ajili ya  kumalizia jengo kwa ajili yaipeleka mbele dini ya kiislamu.

ijitimai hiyo ya kitaifa inatarajiwa kufanyika terehe 22 mwezi 2 mwakani huko kidoto mkoa wa kaskazini unguja.