AKIFUNGUA MAFUNZO KWA WAKUSANYAJI WATAKWIMU WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA

Mtakwimu mkuu  wa serikali   bi  mayasa  mahfoudh  mwinyi amesema  bado kunachangamoto   ya  upatikanaji wa takwimu sahihi  za  makosa  ya  jinai  na  madai   kwa kutokuwa na  mfumo  imara  y a  uwekaji  wa takwimu  ambapo  husababisha   kutolingana  kwa  taarifa  zinazokusanywa.

akifungua mafunzo kwa  wakusanyaji  watakwimu  wa  vikosi  vya ulinzi  na usalama, mahakama  na ofisi  ya  mwendesha  mashtaka  amesema  umefika  wakati  wa  kila  taasisi ya serikali  inakuwa  na kitengo  cha  takwimu  ili kuondosha utoaji wa takwimu  zisizolingana  .

Akielezea  umuhimu wa takwimu  za makosa  ya  jinai na madai  zitatoa tathmini  ya  amani na utulivu  nchini  na  zile  za uhalifu  kuona maeneo  gani yanaripotiwa   ili kuweza kujipanga  kuyadhibiti matokeo  hayo.

naibu  kamishna   chuo  cha  mafunzo  nd ali  abdalla  amesisitiza  ukusanyaji wa  takwimu  uzingatie  vigezo ili  kuweza  kuzipata  zilizo bora  na  zenye  uhalisia  kwa  matumizi.

Wikitoa  michango  yao  washiriki  wa  mafunzo  hayo  wamesema   uchelewaji  wa upatikanaji wa  takwimu  sahihi  ikiwemo  za  udhalilishaji  ndiko  kunakochangia  urudishaji nyuma wa  mapambano  hayo.