AKINAMAMA WA WILAYA YA MASASI NA ZANZIBAR WAMEPONGEZWA KWA USHIRIKI MZURI KATIKA IJITIMAI YA KIMATAIFA

Akinamama wa wilaya ya masasi na zanzibar wamepongezwa kwa ushiriki mzuri katika ijitimai ya kimataifa iliofanyika wilayani humo…
Akifunga ijitimai hiyo mwenyekiti wa jumuiya ya fiysabillah tabligh markaz, amir ali khamis,amesema akinamama wamekuwa mstari wa mbele katika harakati zote tokea hatua ya awali.
Amir ali pamoja na pongezi hizo amewakumbusha waislam kuendelea kuiombea dua nchi ili iondokane na vitendo vya udhalilishaji vinavyowakumba wanawake na watoto.
Baadhi ya waumini hao kutoka zanzibar na masasi wamesema kumalizika kwa ijitimai hiyo kutazidisha kutakasa nyoyo zao kwa kumcha mwenyezimungu katika kutekeleza mambo mema.
Ijitimai hiyo iliofanyika siku tatu ni mashirikiano ya jumuiya ya mtandao wa wanawake wa kiislam kutoka masasi na jumuiya ya fiysabilillah tabligh markaz kutoka zanzibar.