AKINAMAMA WAMETAKIWA KUENDELEZA KUTUNZA AMANI NA UTULIVU ILIYOPO HAPA NCHINI

Akina mama wa chama cha mapinduzi  wa kijiji cha tazari  mkoa wa kaskazini unguja wametakiwa kuendeleza kutunza amani na utulivu iliyopo hapa  nchini ili kuweza kunusuru janga la vifo kwa akina mama na watoto.

Hayo yameelezwa na mwakilishi wa viti maalum mkoa wa kaskazini unguja mhe: panya ali abdalla wakati  akikabidhi seti moja ya tv kwa wanawake wa kijiji cha tazari kwa niaba ya mwakilishi mwezake wa viti maalum mkoa huo  mhe: mtumwa suleiman, amesema nchi hii bado ipo kwenye amani na utulivu uliofanywa kwa busara za viongozi wa nchi yetu hivyo akina mama kunabudi ya kuwaunga mkono viongozi kwa  kuiendeleza amani hiyo.

Kwa upande  wake  mwenyekiti wa uwt mkoa wa kaskazini unguja  bi maryam muharami  amesema tv inaweza kutoa elimu kwa jamii hivyo amewaambia akina mama wa tazari kuitumia tv hiyo kwa kutafutia elimu ili iweze kuwakomboa  katika maisha yao.Nao akina mama hao wamewashukuru viongozi kwa kuwatimizia mahitaji waliyoyataka na kuwaomba kuwatafutia soko la bidhaa zao wanazolima kwani kwa sasa  imekuwa ni changamoto kubwa kwao wao.