AKINAMAMA WANAOJISHUHULISHA NA UVUVI WA CHAZA WAMEIOMBA SERIKALI KUWAJENGEA SOKO

 

Akinamama wanaojishuhulisha na uvuvi wa chaza na uuzaji wameiomba serikali ya mapinduzi ya zanzibar kuwajengea soko la uhakika la kufanya biashara zao ili waweze kuondokana na tatizo la uuzaji wa barabarani.    Wamesema pamoja na jitihada za kufanya biashara ili kuweza kujikwamua na hali za umasikini na kuacha kuwa tegemezi lakini bado biashara hiyo imekuwa haina soko la uhakika . Aidha wamefahamisha kuwa wamekuwa wakikaa karibu na barabara kwa kusubiri wateja,na kuweza kuhatarisha maisha yao.na  kukosewa kugongwa. Zbc katika harakati zake imewashuhudia akinamama hao  pamoja na watoto wao wakiwa karibu na barabara wakiuza biashara hiyo ya chaza.