AKIZINDUA RASMI MASHINDANO YA TAIFA YA MICHEZO YA WATU WENYE ULEMAVU WA AKILI

 

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa wito kwa wazazi wenye watoto walemavu  ambao huwashirikisha watoto wao kwenye michezo tofauti kuchukuwa jitihada za makusudi za kuwaelimisha wazazi wenzao wenye watoto kama hao kuwajumuisha katika michezo na shughuli mbali mbali zinazowahusu.

Amesema michezo mbali mbali wanayoshirikishwa watoto wenye mahitaji maalum mara nyingi husaidia kuleta marekebisho endelevu ya tabia na mienendo ya watu wenye ulemavu wa akili kutokana na kuwa michezo ni tiba.

Akizindua rasmi mashindano ya taifa ya michezo ya watu wenye ulemavu wa akili { special olympics } huko uwanja wa aman mjini Zanzibar Balozi Seif amesema wananchi lazima wabadili misimamo na mitazamo yao jinsi wanavyowaona na kuwachukulia watu wenye ulemavu wa akili.

Balozi Seif alisema walemavu ni binaadamu kama walivyo wengine  ambao wana uwezo na hata vipaji vya kufanya mambo mengi makubwa na ya ajabu endapo watapatiwa fursa za kutumia vipaji na ujuzi waliobarikiwa.

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar alisema kupitia mashindao ya michezo mbali mbali ya kimataifa ya watu wenye ulemavu vijana wa tanzania wamekuwa wakililetea sifa taifa kutokana na ushiriki wao uliowawezesha kuibuka na medali mbali mbali kwenye mashindano hayo.

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar aliwashukuru na kuwapongeza waandaaji wa mashindano ya michezo ya watu wenye ulemavu wa akili kwa jitihada walizochukuwa za kuwashindanisha wanamichezo hao licha ya changamoto nyingi walizopambana nazo ikiwemo ukosefu wa wadhamini na wafadhili wa kutosha.

Akitoa taarifa ya mashindano hayomkurugenzi wa special olympics tanzania chales rais alisema michezo hiyo imeanzishwa katika misingi ya kuwaandaa watu wenye ulemavu hasa watoto kushiriki katika matukio na shughuli za amali kama watu wengine.

Hata hivyo charles alieleza kwamba bado ipo changamoto kubwa inayowakabili watu wenye ulemavu wa akili ya unyanyapaliwa kutoka kwa baadhi ya watu na hatimae unapelekea kukoseshwa haki zao za kupata elimu, ushiriki wa michezo sambamba na mchanganyiko ndani ya jamii  katika mazingira ya kutafuta maisha.

0 akimkaribisha mgeni rasmi kuyazindua mashindano hayo ya watu wenye ulemavu wa akili mwenyekiti wa special olympics tanzania  dr. Mwanandi swed  aliziomba serikali zote mbili nchini tanzania kuandaa bajeti maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa akili ili zisaidie harakati zao za kila siku ikiwemo shughuli za michezo.

Dr. Mwanandi alisema hicho ni kilio cha muda mrefu kinacholiliwa na kundi la watu wenye mahitaji maalum hasa lile ya michezo ya olympics ambapo halijawa kupatiwa fungu ndani ya bajeti za taasisi za umma tokea kuasisiwa kwa michezo hiyo mnamo mwaka 1988.

Zanzibar ina dv uteuzi waziri 7 disemba 2017

Wziri wa nchi afisi ya rais tawala za mikoa, serikali za mitaa na idara maalum za smz mh. Haji omar kheir amefnya uteuzi wa wajumbe wa tume ya utumishi ya idara maalum za smz.

Walioteliwa ni kepten mstaafu feteh saad mgeni, luteni kanl mstaafu mohamed abdalla rex, cdr khatibu ali hamdu na kepteni khamis simba khamis.

Wengine ni dcf gora haji gora, dcp Dkt. Haji hamdu omar, luteni kanl mussa mohamed shaame na meja yussuf khamis yussuf.