AKIZINDUA ZOEZI LA UPIMAJI WA AFYA

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali mh. Riziki pembe juma amesema  jitihada za serikali ya  mapinduzi ya zanzibar katika kumkomboa mwanamke zinaonesha kupiga  hatua nzuri katika nyanja tofauti  nchini.

Akizindua zoezi la upimaji wa afya  lililoandaliwa na jumuiya rafiki wa wanawake na watoto  kwa ushirikiano na kampuni ya dina foundation  katika kijiji cha dole  kufuatia  siku ya wanawake duniani,  mh. Riziki  amesema  maendeleo ya mwanamke yamefikia pahala pazuri kwani  tayari wamepata mwamko  kwa kujishughulisha  na masuala mbalimbali ya  kiuchumi  jambo  ambalo limewaondoa katika  tatizo la utegemezi.

Nae mjumbe wa jumuiya hiyo bibi asha salum bakar amesema  wanawake wengi walikuwa wanadhalilika na watoto wao majumbani  sababu iliyowafanya kujikusanya pamoja na kuunda jumuiya hiyo kwa lengo la kuwaelimisha wanawake wenzao  ili waweze kujinasua na hali hiyo.

Wakaazi wa maeneo hayo wameelezea kufarajika na hatua hiyo  ambayo  imewasaidia kupata matibabu ya bure.

Jumla ya wakaazi 250  wanatarajiwa kupatiwa  huduma za kupima afya zao   pamoja na kupatiwa  matibabu kwa watakao gundulika  kuwa  na matatizo yakiwemo ya  sukari, presha na kifua.