AKIZUNGUMZA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE

Ubalozi mdogo wa china uliopo zanzbar umesema unaunga mkono jitihada za wanawake wa zanzibar kwa kushiriki kikamilifu katika harakati za kimaendeleo za kitaifa na za kijamii.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kwenye jengo la ubalozi mdogo wa china uliopo mazizini, mke wa balozi mdogo wa china bi liu jie, amesema wanawake wa china wamekuwa na utaratibu kama huo wa wenzao wa zanzibar, hasa kujitolea katika kutoa elimu inayoimarisha utamaduni wa nchi mbili hizo, na kuchangia ongezeko la uchumi wa taifa lao.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, waziri wa kazi, uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto, mh. Moudlin castico, amesema zanzibar na tanzania kwa ujumla zimeongeza fursa za nafasi za uongozi kwa wanawake, na kuwajengea uwezo wa kitaaluma na kuwapatia mbinu bora za ujasiriamali.

Hafla hiyo imeambatana na chakula cha usiku pamoja na maonesho ya tamaduni za china.