AKIZUNGUMZA NA ERDOGAN WALIPOKUTANA KATIKA MJI MKUU WA UTURUKI

 

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Uturuki  Recep Tayyib Erdogan wamepinga vikali uamuzi wa marekani kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa israel.

Katika ziara fupi eneo la mashariki ya kati akiwa nchini uturuki putin  amesema uamuzi wa marekani unahatarisha usalama katika eneo hilo.

Kabla ya kutua mjini ankara hapo jana kuonana na erdogan, putin amefanya ziara ya kushtukiza kwa kuitembelea syria ambapo amevitaka vikosi vyake kuachia silaha na amepanga kufanya mazungumzo na rais wa misri abdel fattah el-sisi kuhusu amani ya eneo hilo.

Katika ziara yake ya kanda hiyo putin ameongeza mikataba baina ya nchi yake na rafiki zake wa mashariki ya kati.

Akizungumza na erdogan walipokutana katika mji mkuu wa uturuki rais putin amesema hadhi ya mji wa jerusalem inapaswa kuzungumzwa na wenyewe palestina na israel.

Ziara hiyo imekuja wakati hasira ikiongezeka katika ulimwengu wa kiislamu juu ya uamuzi wa rais donald trump kuutambua mji wa jerusalem kuwa mji mkuu wa israel, ambapo pia sera hizo za marekani zimepingwa na hata na washirika wake