ALIYEKUWA KATIBU TAWALA WILAYA YA WETE AMEZIKWA JANA

Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na idara maalum za smz mh. Haji omar kheir ameungana na viongozi na wananchi wa kisiwa cha pemba katika mazishi ya marahemu mussa ali muhamed aliyekuwa katibu tawala wilaya ya wete aliyezikwa katika kijiji cha kiwani wilaya ya mkoani.

Akitowa mkono wa pole kwa familia na wanachi mh. Haji amesema msiba huo umeugusa serikali na viongozi wenzake na sio kwa famila, jamaa na rafiki wake wa karibu.

Akisoma wasfu wa marehemu huyo katibu tawala wilaya ndogo kojani makame amesema marehemu ameanza kuitumia serikali katika wizara ya bahari mwaka 1993 na aliteuliwa kuwa katibu tawala wilaya ya wete mwaka 2015 na ameacha kizunka mmoja na watoto nane.

Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amin.