ALIYEKUWA WAZIRI MKUU WA LEBANON SAAD HARIRI AMEKUBALI MWALIKO WA KWENDA NCHINI UFARANSA

 

Aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri amekubali mwaliko wa kwenda nchini ufaransa, baada ya lebanon kuituhumu Saudi Rabia kwa kumzuia kufuatia hatua yake ya kujiuzulu.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa amethibitisha hilo wakati alipofanya mazungumzo  na mwana mfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman.

Amesema Hariri pamoja na familia yake watawasili ufaransa katika siku chache zijazo na wamealikwa kwa ajili ya kukaa nchini humo kwa siku chache lakini amesema sio kwamba kiongozi huyo amepewa hifadhi ya kisiasa.

pia rais wa nchi hiyo emanuel macron ameongeza kuwa hariri atapaswa kurejea lebanon kuthibitisha mwenyewe kujiuzulu kwake au kuubatilisha uamuzi huo.

Rais wa Lebanon michel aoun anaituhumu Saudi Arabia kwa kumzuia Hariri na amekataa ombi lake la kujiuzulu akiwa ng’ambo.