AMESEMA KILA MMOJA ANA HAKI YA MATUMIZI YA ARDHI KWANI KINACHOTAKIWA NI KUFUATA SHERIA

 

Mkuu wa wilaya ya magharibi b kepteni silima haji haji ameziagiza idara ya ardhi na baraza la manispaa magharibi b kuyaangalia maeneo ya wazi ambayo umiliki wake unautata kuyafatilia na kuona yanafuata taratibu za kisheria katika umiliki ili kuondoa migogoro inayoweza kuepukika.

Amesema kila mmoja ana haki ya matumizi ya ardhi kwani kinachotakiwa ni kufuata sheria ambazo zinaelekeza matumizi bora ya ardhi kama yanavyoelekezwa na idara ya ardhi.

Mkuu huyo wa wilaya alikuwa akikagua eneo la kiembesamaki uwanja wa ndege lenye mzozo wa umiliki katika ghala la bi zainab diria kwa kupitishwa bomba la maji ambapo anadai eneo hilo halistahili kupitishwa bomba hilo.

Amesema serikali haina nia ya kutaka kumpokonya mtu eneo lake bali ni kutaka kufuata taratibu za kisheria ili shughuli za kimaendeleo ziendelee kufanyika kama zinazotaka kufanywa katika eneo hilo.

Kwa upande wake mmiliki wa ghala hilo bi zainab diria amesema hakatai kufanyika kwa shughuli hiyo bali kinachokwamisha ni kutokuwepo tena kwa njia ya uingizaji na utoaji wa gari kwa ajili ya kuleta mizigo.