AMESEMA KUMEJITOKEZA HOFU KWA BAADHI YA WATENDAJI WA SEKTA

Mkuu  wa  mkoa  kusini  unguja, mh. Idrissa  muslim  hijja, amewataka  watendaji  wa  ofisi  za  halmashauri  na  wananchi, kutokuwa  na  hofu  ya  mfumo  wa  kupekekwa  madaraka  mikoani ugatuzi, kwani  umefanyiwa  utafiti  wa  kutosha na kwamba  utafanikiwa.

Amesema  kumejitokeza  hofu  kwa  baadhi  ya  watendaji  wa  sekta  zilizopeleka  madaraka katika  serikali  za  mitaa, kwamba  watapoteza  nafasi  zao  za  kazi jambo  ambalo sio  la  kweli.

Akifungua  mafunzo  kwa  watendaji  wa  vikosi  kazi  vitano  vya  utekelezaji  wa  malengo  ya  sera  ya  ugatuzi, mh. Hijja, amesema  jitihada zinaendelea  kufanyika  za  kutoa  elimu  kwa  kushirikisha  wataalamu  ili  kuona  mpango  huo  serikali  unafanikiwa.

Akiwasilisha ripoti  ya  utekelezaji  mjumbe  wa  kikundi  kazi  masuala  ya  fedha, nd. Haji  ali  haji, amesema  wametayarisha  mpango  kazi  kwa  kujifunza  kwa  baadhi  ya  nchi  zilizopata  mafanikio  kupitia  ugatuzi.

Mtaalamu  ushauri  rasilimali  watu, richard  kimey  pamoja  mtaalamu  rasilimali  fedha, gikene  john, wameshauri  kuandaliwa  sheria  madhubuti  na  kanuni  za  kusimamia suala  ugatuzi  ili  kuepusha  migongano  ya  kiutendaji.