AMEUPONGEZA UONGOZI WA JIMBO LA DONGE KWA MASHIRIKIANO MAZURI

 

Mkuu wa wilaya ya kaskazini B Rajab Ali Rajab ameupongeza uongozi wa jimbo la donge kwa mashirikiano mazuri waliyoyatoa kwa  taasisi ya ZARDEFO FOUNDATION na kupelekea kukamilika kwa ujenzi wa kisima cha maji safi na salama katika kijiji cha mkuyuni shehiya ya mkataleni.

Ameeleza hayo katika hafla ya ufunguzi wa kisima cha maji uliofanyika katika kijij hicho ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa maji safi na salama ambao  lilikuwa likileta usumbufu mkubwa hasa kwa kina mama na kushindwa kushiriki katika shughuli za kimaendeleo

Akizungumza mkuu wa wilaya ya kaskazini B Rajab Ali Rajab amesema wilaya yake inakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa huduma hiyo kwa baadhi ya maeneo kutokana na kuwepo kwa baadhi ya matatizo katika visima vya maji jambo ambalo linaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi

Amesema kitendo cha taasisi ya zardefo foundation kupeleka huduma hiyo ya maji ni kitendo cha kupongezwa na kuungwa mkono na wadau wa maendeleo ili kwenda sambamba na malengo ya serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi wake ikiwemo huduma ya maji safi na salama.          Akitoa neno la shukran kwa niaba ya uongozi wa Zardefo Faundation Ali Muhammed Hji amewashukuru wakaazi wa kijiji hicho kwa ushirikiano wao kuanzia ujenzi wa kisima hicho hadi kukamilika kwake

Kwa upande wao wakaazi wa kiji cha mkuyuni wameushukuru uongozi wa jimbo pamoja na taasisi ya zardefo faundation kwa kuamua kwenda kupeleka huduma hiyo muhimu na kuahidi kuitunza miundombinu ya kisima hicho.