AMEWATAKA VIJANA KUWACHA KUKEBEHI JUHUDI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI ZA KUWAINUA

Mkuu wa Wilaya ya kaskazini “A” Hassan Ali Kombo amewataka vijana kuwacha kukebehi juhudi zinazofanywa na  serikali za kuwainua vijana kiuchumi na badala yake wafanye juhudi za kuzifikia fursa zinazotolewa na serikali yao.

Akizungumza na wajumbe wa  mabaraza ya vijana katika mafunzo ya kuimarisha mabaraza hayo yaliyoandaliwa na asasi za kiraia za mkoa wa kaskazini unguja mkuu huyo amesema serikali imeandaa mambo mbalimbali ya kuwasaidia vijana katika kujiendeleza kimaisha pamoja na kuandaa sera ya mabaraza  lakini anashangaa kusikia kiongozi akiwa kwenye baraza la vijana  hajui juhudi zinazofanywa na serikali juu ya mabaraza  hayo.

Kwaupande wake mkufunzi wa mafunzo hayo Nd: Abdalla Mussa Hija amewashauri wajumbe hao kuwa tayari  kufanya kazi katika kuyaimarish mabaraza ya vijana pamoja na kuishauri serikali katika mambo ya maendeleo kwa vijana.

Nao wajumbe waliopatiwa mafunzo ya ujasiliamali na mtandao wa Asasi za kiraia mkoa wa kaskazini unguja huko morogoro wameelezea mafanikio ya ziara yao.