AMNESTY INTERNATIONAL LIMEMSHUTUMU RAIS WA MAREKANI

Shirika la kimataifa la haki za binaadamu, amnesty international limemshutumu rais wa marekani donald trump na viongozi wengine nchini uturuki, hungary na ufilipino.
Shirika hilo limesema viongozi hao wamewatumia vibaya wakimbizi, kwa manufaa yao ya kisiasa, badala ya kutatua tatizo lililowafanya kuyakimbia mataifa yao.
Katika mwaka 2016 amnesty limeeleza ulikuwa mwaka mbaya kwa haki za binaadamu, ambapo uhalifu wa kivita umefanyika duniani kote.
Ripoti hiyo inapinga sera ambazo zinakubalia ubaguzi wa rangi na chuki.