ANGELLAH KAIRUKI AMEZINDUA BODI YA PILI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA UTUMISHI WA UMMA.

Waziri wa nchi, ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora angellah kairuki amezindua bodi ya pili ya mishahara na masilahi katika utumishi wa umma.
Akizungumza kabla ya uzinduzi wa bodi hiyo waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa ummma angellah kairuki amesema serikali ya awamu ya tano inaendelea na mchakato wa kuboresha maslahi ya watumishi wa umma na kuzishughulikia kero zao.
Naye mwenyekiti wa bodi hiyo donald ndagula amesema bodi itahakikisha inashughulikia maslahi ya watumishi wa umma bila kuwabagua.
Bodi hiyo imeundwa kufuatia kuwapo kwa malalamiko ya muda mrefu ya watumishi wa umma juu ya mishahala yao na tofauti iliyopo baina ya viwango vya mshahara kwa watumishi waliokuwa na viwango sawa vya elimu, bodi hiyo inaundwa na wajumbe saba na inaongozwa na mwenyekiti wake kamishna mstaafu wa idara ya uhamiaji donald ndagula.