ASASI ZA KIRAIA ZINANAFASI KUBWA KATIKA KUWASHAJIHISHA WANANCHI KATIKA KUTELEKEZA MAENDELEO

Mwakilishi  wa shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa –UNDP-Zanzibar  Rukiya Wadoud amesema asasi  za kiraia zinanafasi kubwa katika kuwaelimisha na kuwashajihisha wananchi kushiriki katika kutelekeza malengo ya maendeleo endelevu.

Akizungumza na viongozi wa shehia, dini na watu mashuhuri wa Wilaya ya Micheweni , Rukiya Wadoud amesema ili malengo hayo yaweze kufanikiwa ,lazima kuwepo na ushirikiano wa viongozi kutoka asasi mbali mbali.

Mapema akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Mtadao wa Asasi za Kiraia Zanzibar –ANGOZA- , Asha Aboud Mzee amewataka viongozi hao  kutumia nafasi kuihamasisha jamii kushiriki kutelekeza malengo ya maendeleo endelevu.

Kwa upande wao viongozi wa dini akiwemo Mohammed Nassor Khamis na John Shimba Shija wameahidi kuifikishia jamii elimu waliyoipata ili kuona wanashiriki kikamilifu katika kutekeleza malengo hayo.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App