ASILIMIA KUBWA YA WANANCHI WA ZANZIBAR WANAFAIDIKA NA MATUNDA YA ELIMU

Zaidi ya shilingi milioni kumi na tano zimekusanywa katika matembezi ya hisani kwa ajili ya kutafuta fedha za ujenzi wa chuo cha ualimu huko bububu.
Matembezi hayo yaliyowashirikisha walimu ,wanafunzi wa na viongozi yalianzia beit el ras hadi skuli ya bububu nje kidogo ya mji wa zanzibar.
Akizungumza mara baada ya matembezi hayo katibu mkuu wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi ndugu joseph abdalla meza amewataka wananchi kujitolea katika kujenga nchi yao na suala la misaada ya wafadhili liwe ni la matokeo tu.
Amesema asilimia kubwa ya wananchi wa zanzibar wanafaidika na matunda ya elimu na kutaka vizazi vijavyo viandaliwe mazingira mazuri ya kupata elimu.
Katika hafla hiyo mgeni wa heshima pia alikabidhi vyeti kwa walimu waliohitimu mafunzo ya ualimu waliomaliza hivi karibuni.