Recent Posts by Fatma Muhamad

WASANII NCHINI WAMETAKIWA KUSAJILI VIKUNDI VYAO ILI KUFAIDIKA NA FURSA ZITAKOZOJITOKEZA

Baraza la Sanaa,Sensa ya Filamu na Utamduni Zanzibar limewataka Wasanii mbalimbali Nchini kusajili vikundi vyao ili kufaidika na fursa zitakazojitokeza ndani na nje ya nchi katika kukuza kazi zao.

Akizungumza na wasanii wa Wilaya ya Kati katika mafunzo kwa wasanii hao katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu  na Utamaduni Zanzibar Dk Omar Abdallah Adam amesema ili msanii au kikundi cha wasanii kufikia mafanikio anawajibu wa kujisajili katika taasisi husika kwa ajili ya kunufaika na fursa zinazojitokeza kwa wasanii hao.

Amesema miongoni mwa fursa ambazo msanii anaweza kuzipata baada ya kujisajili  ni kushiriki katika matamasha mbali mbali ya ndani na nje, kukuza kipato cha wasanii na kuweza kupatiwa elimu kwa mujibu wa mabadiliko yaTekenolojia Duniani.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo wameelezea kufurahishwa na mafunzo waliopatiwa kwani yatawajengea uwezo wa kujiamini wakati wa uwasilishaji wa kazi zao  kwa jamii

WAJASIRIAMALI WA MATUNDA NA MBOGA MBOGA KISIWANI PEMBA WAMETAKIWA KUZALISHA KWA WINGI BIDHAA ZAO

Wajasiriamali wa matunda na mboga mboga kisiwani Pemba wametakiwa kuzalisha kwa wingi bidhaa zao pamoja na kuzalisha bidhaa zilizo bora ili kuyafikia masoko ya ndani na nje ya nchi.

Wito huo umetolewa na kaimu Afisa Mdhamin Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee  Wanawake na Watoto Hakimu Vuai Shein huko Gombani wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya awali kabla ya kupewa mikopo kwa wajasiri amali hao

Kwa upande wake kaimu mratibu  mfuko wa uwezeshaji Haji Khamis Haji amesema Mfuko huo unalengo la kuwawezesha wananchi wake hasa kipato cha chini pamoja na  kuwataka fedha hizo waweze kuzirudisha kama walivyopangiwa

Nao wajasiri amali hao wamesema watahakikisha watayatumia taaluma  waliyopewa  ili waweze kufikia malengo yao .

Jumla ya sh millioni ishirini zinatarajiwa kutolewa kwa wajasiri amali thalathini na tisa wakiwemo wanawake kumi na saba na wanaume ishirini na mbili.

HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA KWA MTUMISHI ATAEBAINIKA KUZOROTESHA MIRADI YA WANANCHI

Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh Mmanga Mjengo Mjawiri, amesema atahakikisha anamchukulia hatua za kisheria mtumishi yeyote atayebainika kudhorotesha Shughuli za miradi ya maendeleo ya Wananchi.

Mh. Mmanga ameyasema hayo huko katika bonde la umwagiliaji Machigini, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.

Mh. Mmanga amesema kuwa, kuna baadhi ya watendaji wamekuwa wakisimamia miradi yao kipindi cha mwisho cha mkataba kwa malengo ya kufanya ubabaifu huku huduma zikisuasua bila maelezo yamsingi.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa kuongeza tija kwa wakulima (ERPP) katika bonde la Machigini Afisa MkuuIdara ya Umwagiliaji, Mbarouk Ali Mgau, amesema ni kipindi cha miezi sasa tokea kukamilisha malipo kwa shirika la umeme lakini bado hawajapatiwa huduma, hali inayodhorotesha shughuli za   wakulima wa bonde hilo.

Kwa upande wao wakulima wa bonde hilo, wamesema kuwa, kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la umeme ambao ungaliwasaidia katika kuvutia maji ndani ya bonde lao pamoja na ubovu wa miundombinu ya umwagiliaji.

WAJUMBE WA BLW WAMEIPONGEZA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE KWA KUVIIMARISHA VIWANJA HIVYO

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Mh. Mwinyihaji Makame Mwadini ameipongeza mamlaka ya viwanja vya ndege kwa kuviimarisha viwanja hivyo na kuwa vyenye hadhi na kuhakikisha usalama wa abiria na mali zao.

Akizungumza katika  ziara ya kuyatembea maeneo ya viwanja hivyo pamoja na kuona shuhuli zao ameelezea kuridhishwa na  hatua kubwa zilizochukuliwa na mamlaka hiyo ili kuzidi kuwavutia wageni wanaoingia na kutoka nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Vdege Bi Zaina Ibrahim amesema hivi sasa wapo katika utekelezaji wa mradi wa ufungaji vipoza hewa ili kuweza kumalizia ufungaji wa mashine ya exray ili kurahisisha ukaguzi wa mzigo ya wanaoingia nchini.

Kwa upande wake Mratibu Mwandamizi wa Mhamiaji Bakari Mohamed Ameir amesema mfumo uliopo hivi sasa wa Elektroniki viza utasaidia kwa kiasi kikubwa ongezeko la mapato nchini kutokana na wageni wanaokuja moja kwa moja kutoka nchini mwao kuingia nchini.

Recent Comments by Fatma Muhamad

No comments by Fatma Muhamad yet.

Powered by Live Score & Live Score App