Recent Posts by Fatma Muhamad

USHIRIKISHWAJI WA WADAU KATIKA UANDAAJI WA SERA YA HABARI UTASAIDIA KUPATIKANA SERA MADHUBUTI

Imeelezwa kuwaUshirikishwaji wa Wadau Katika Uandaaji wa Sera ya Habari Utasaidia Katika Kupatikana kwa Sera Madhubuti ya Habari Nchini

Hayo Yameelezwa na Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii na Mambo yaKale Pemba Khatibu Jjuma Mjaja kwa Niaba ya Naibu Katibu Mkuu Habari Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Alipokuwa Akifungua Kkutano wa Wadau Mbali Mbali wa Kujadili Sera ya Habari Uliofanyika Ukumbi waSanaa Rahaleo.

Amesema Wadau wa Habari Pamoja na Wananchi ni Watu Muhimu Ambao Michango yao Itasaidia Katika Kupatikana kwa Sera Madhubuti.

Akiwasilisha Sera ya Habari Katika Mkutano Huo Afisa Mipango Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Nd Amina Omar Amesema Miongoni Mwa Malengo Makuu ya Mabadiliko ya Sera Hiyo ni Kujenga Umoja na Ushirikiano kwa Wananchi Ili Kuleta Maendeleo Katika Tasnia yaH abari.

Wakichangia Katika Mkutano HuBaadhi ya Wadau waHabariWamesema IpoHaja  kwa Sera Hiyo KuandaaUtaratibu Maalum wa Kuviimarisha Vyombo Binafsi Pamoja na Waandishi Wao Juu ya Maslahi Bora Yenye Tija .

 

SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR LIMEANZA KUWEKA MASHINE ZA UKAGUZI WA ABIRIA NA MIZIGO

Shirika la Bandari Zanzibar Limeanza Kuweka Mashine za Ukaguzi wa Abiria na Mizigo katika Bandari ya Malindi kwa Abiria Wanaoingia WakitokeaTtanzania Bara.

Aidha Shirika Hilo Tayari Limeshaweka Mashine kamaHizo Katika Bandari ya Mkoani Kisiwani Pmba kwa Ajili ya Kuimarisha Hali Usalama.

Hayo Yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe, Mohammed Ahmada Salum Kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi Wakati Akijibu Swali la Mwakilishi waJimbo la Chake Chake Mhe, Suleiman Sarahani Aliyetaka Kujua Hali ya Usalama katika Bandari Hhizo.

Aamesema Utekelezajio wa Kazi Hiyo Una Mafanikio Makubwa Kwani Usalama wa Abiria,Mizigo na Cchombo Wanachopanda ni wa Uhakika.

Wakati Huo Huo Waziri wa Kilimo Maliasili ,Mifugo na Uvuvi Mhe ,Rashid Ali Jjuma Amesema Mabanda Yaliyojengwa kwa Ajili ya Afisi katika Mabonde ya Kilimo cha Mpunga waUmwagiliaji Yatafanyiwa Matengenezo Sambamba na Uchimbaji wa Visiwa Vingine kwa Aajili ya Kuimarisha Kilimo cha Umwagiliaji.

Katika Hatua Nyinge Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Amewasilisha Ripoti ya Kamati Hiyo katika Kijkao cha Baraza Hilo Kinachoendelea Huko Chukwani.

 

HALI YA USAFI KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MJI WA ZANZIBAR YAMEKUWA HAYARIDHISHI

Hali ya Usafi Katika Baadhi ya Maeneo ya Mji wa Zanzibar Yamekuwa Hayaridhishi Kutokana na Baadhi ya Watu Kupinga Sheria ya Utunzaji wa Mazingira.

Hayo Yamebainika BaadaKufanya Zoezi la Usafi wa Mazingira katika Maeneo ya Fukwe za Bahari ya Forodhani Ambapo Baadhi ya Wadau wa Mazingira Wamesema Kuendelea kwa Uchafuzi wa Mazingira Kunaweza Kutahatarisha Maisha ya  Wanadamu na  Viumbe Wengine wa Baharini.

Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi Marina Joel Thomas  Amesema si Vyema kwa Wanachi Kufanya Uchafu  Hasa katika Maeneo ya Fukwe za Bahari  Ambapo Kufanya  Hivyo Kunaweza  Kupunguza Idadi ya Watalii Wanaoingia  Nchini na Kuikosesha Serekali  Mapato.

Akizungumzia Juu ya Ujaji wa Boti  Iliotengenezwa  kwa Malighafi ya Plastik Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Mjini Nd Saidi Juma Ahmada  Amewataka Wananchi kuwa na Tabia ya Kuiga Mambo  ya Maendeleo .

Zoezi Hilo la Usafi wa Mazingira katika Maeneo ya Fukwe Yamewashiriksha Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Serekali, Washiriki Kutoka Kampuni ya Danause na Watendaji wa Serekali.

WANANCHI WAMEISHUKURU SERIKALI KWA UJENZI WA BANDA LA KUSUBIRIA WAGONJWA

Wananchi Kutoka Maeneo Mbali Mbali Wameishukuru Serikali Kupitia Wizara ya Afya kwa Ujenzi wa Banda la Kusubiria Wagonjwa Katika Hospitali Kuu ya Mmnazi Mmoja.

Wakizungumza kwa Nyakati Tofauti Wananchi Hao Wamesema Kumalizika kwa Ujenzi Huo Kutawawezesha Kukaa Katika Eneo Yenye Stara Tofauti na Sasa Ambapo Wanakaa Sehemu Yoyote Wakisubiri Muda wa Kuangalia Wagonjwa.

Akizungumza na Zbc Msemaji wa Hospital  Hiyo Hassan Makame Mcha   Amesema Wamelazimika Kujenga Banda Hilo Kutokana na Malalamiko ya Wananchi Wanaokuja Kusubiri Wagonjwa wao Ambao Hulazwa  katika Hospitali Hiyo Ambapo Wengi wao Wanatoka Maeneo ya Nje ya Mji.

Amesema ujenzi huo utakapo Malizka Kutakuwa na Maeneo aalum ya Kulala Watu wanaosubiri wagonjwa wao na kuondoka na hali iliyopo hivi sasa kulala katika wodi wakati unapokuwana wagonjwa.

Amesema Ujenzi Huo Unatarajiwa Kumalizika Mwezi Ujao Umegharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 30 na Utachukua Wananchi Zaidi ya 150.

Recent Comments by Fatma Muhamad

No comments by Fatma Muhamad yet.

Powered by Live Score & Live Score App