BAADHI YA WANAUME KUTOTOA MASHIRIKIANO KWA KINA MAMA KUHUSU UZAZI WA MPANGO

 

 

Baadhi ya Wanaume kutotoa mashirikiano kwa kina mama kuhusu uzazi wa mpango na Afya ya mama na mtoto ni moja ya tatizo linalosabaisha Zanzibar kuendelea kuwa na vifo vitokanavyo na uzazi.

akizungumza na waandishi wa habari meneja  kitengo shirikishi cha afya ya uzazi wa mama na mtoto Dk. Mtumwa Ibrahim amesema wanapambana na tatizo hilo kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu katika jamii.

Afisa uhamasishaji wa afya ya uzazi na matumizi ya njia za uzazi wa mpango tatu ahmada ali na kassim kirobo wamesema kuna baadhi ya kinamama hutumia njia za uzazi wa mpango bila ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu.

nao waandishi wa habari wamekishauri kitengo hicho kubadilisha mfumo wa utoaji wa elimu ili kupatikana kwa mafanikio na wanaume kushirikishwa kikamilifu katika mpango huo.