BAADHI YA WATU WANAOZITUMIA KAZI ZA WASANII KWA NJIA ZA HADAA KWA MASLAHI YAO BINAFSI

Waziri wa habari utalii utamaduni na michezo mh rashid ali juma amesikitishwa na baadhi ya watu wanaozitumia kazi za wasanii na wabunifu mbalimbali kwa nji za hadaa kwa maslahi yao binafsi.

amesema vitendo hivyo haviwezi kufumbua macho katika kuhakikisha haki za wasanii zinalindwa kwa maslahi ya msanii mwenyewe kwa vile wametumia ujuzi wao mkubwa kufanya kazi hizo.

akizungumza na mtunzi maarufu wa mashairi Zanzibar Haji Gora haji  alipomtembelea nyumbani kwakwe bububu melinane anaelalamika kudhulumia haki zake za kisanii amesema atahakikisaha Wizara hiyo inalipatia ufumbuzi wa haraka swala hilo  kwa kuwa ina jukumu la kulinda kazi za wasanii.

mmoja watoto wa mzee gora amesema baba yake hakuwahi kufaidika juu ya kazi yake ya sanaa ya utunzi wa mashairi na vitabu badala  yake amejitokeza mtu na kujimilikisha haki zote za kitabu alichokitunga mzee gora kiitwacho maisha ya haji Gora bila ya kushirikisha familia ya mzee huyo.