BAADHI YA WAZEE KATIKA KIJIJI CHA BUMBWINI WAMETHIBITIKA KUUGUWA MARADHI YA FISTULA

 

Mratibu wa maradhi ya fistula zanzibar bi aziza faki silima, amesema  baadhi ya wazee katika kijiji cha bumbwini mafufuni wamethibitika kuuguwa maradhi ya fistula.Amesema wazee hao wamefanyiwa uchunguzi wa kina  na kuonekana kweli wanakabiliwa na maradhi hayo.

Akizungumza na zbc aziza amesema mipango inaandaliwa ya  kuwafikisha wazee hao jijini dar es salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya maradhi hayo.Amewafahamisha wananchi kwamba  ugonjwa  huo sio wa kutisha sana kwani mgonjwa anaweza kupona endapo atafanyiwa matibabu yanayostahili. Mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm taifa  leila burhani,amesema hatua hiyo ya kumpeleka mtaalamu huyo kwa wazee hao ilikuwa na lengo la kuwachunguza ili kuona kama wana maradhi ya festula  au laa.