BALOZI SEIF AMEHUDHURIA MAONYESHO YA 15 YA KIMATAIFA YA BIASHARA KATIKA JIMBO KA GUANGXI

 

makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi amesema uwepo wa tanzania katika maonyesho ya 15 ya kimataifa ya biashara katika jimbo ka guangxi ni ishara ya utekelezaji wa dhati wa sera ya uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya tanzania na china.
amesema sera hiyo ya uhusiano  ni ndoto iliyokuwemo ndani ya  nyoyo za viongozi waasisi wa mataifa hayo mawili marehemu mwalimu julius  nyerere na mwenyekiti wa chama cha kikoministi cha china marehemu mao zedong  wakati wakiotesha mmea wa ushirikiano wa pande hizo mbili.
balozi seif ali iddi alitoa kauli hiyo wakati wa akilizindua rasmi banda la tanzania kwenye maonyesho ya 15 ya kimataifa ya biashara { china asean expo 2018 } yanayotarajiwa kufunguliwa kesho katika mji wa nanning nchini jamuhuri ya watu wa china.
alisema juhudi kubwa iliyochukuliwa na waratibu wa maandalizi ya maonyesho hayo ya kuwawezesha wafanyabiashara, na wajasiri amali wa tanzania wanashiriki vyema kwenye maonyesho hayo imezingatia vyema urafiki wa karibu wa kiuchumi na kiutamaduni unaoendelea kuziunganisha pande hizo mbili.
balozi seif alieleza kwamba banda la tanzania lililokusanya vitu mbali mbali vinavyoashiria uwepo wa vivutio vya uwekezaji ukiwemo mlima mrefu barani afrika wa kilimanjaro litawasaidia watu wa bara za asia kuielewa tanzania na rasilmali zilizomo ambazo zinaweza kutoa fursa kwao kuwa  na nia ya kutaka kuwekeza.
makamu wa pili wa rais wa zanzibar alifahamisha kwamba jamuhuri ya muungano wa tanzania imebarikiwa kuwa na maumbile mazuri ya asili hasa kutokana na hifadhi za wanyama na misitu ikiwa kivutio kikubwa kinachotoa fursa kwa wageni mbali mbali duniani kuangalia maumbile hayo.
alisema asilimia 25% ya ardhi ya tanzania imezunguukwa na maeneo ya hitadhi yanayotoa taswira ya kuunganishwa kwa safari za kitalii katika bara la afrika yakiunganishwa sambamba na mlima maarufu ya kilimanjaro uliopo kaskazini mwa nchi.
akizungumzia fursa za utalii zilizopo katika visiwa vya marashi ya karafuu vya zanzibar  ambavyo ni sehemu ya jamuhuri ya muungano wa tanzania makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif alisema zipo fukwe za kuvutia,kima adimu duniani pamoja na bidhaa za viungo vitu vinavyompa mapumziko ya raha mgeni au mtalii anayeamua kuvitembelea.
balozi seif alisema mji mkongwe wa zanzibar uliojumuishwa katika urithi wa kidunia kwa miaka kadhaa sasa chini ya usimamizi wa shirika la sayansi, elimu na urtamaduni la umoja wa mataifa {unesco} umekuwa sehemu ya mafunzo kwa watalii hasa wataalamu wa masuala ya historia wanaofanya utafiti na kukamilisha tafiti zao.
akizungumza na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari vinavyoripoti kiswahili balozi seif  yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye maonyesho hayo  ambayo yameonyesha dalili ya kuzisaidia nchi za afrika kutangaza soko.
balozi seif alisisitiza wakulima wa bara la afrika kuongeza bidii katika uzalishaji wa zao la muhogo ambalo linahitajika kwa wingi nchini jamuhuri ya watu wa china.
alisema takwimu zinaonyesha wazi kwamba mahitaji ya chakula cha muhogo nchini china yanakadiriwa kufikia tani 50 kwa mwaka.
akitoa maelezo mafupi mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya biashara tanzania {tan trade} nd. edwin novath rutageruka alisema jumla ya makampuni 20 kutoka tanzania bara na zanzibar wameshiriki maonyesho hayo.
mkurugenzi rutageruka alisema makampuni hayo yamejumuisha wafanyabiashara, wajasiri amali pamoja na baadhi ya taasisi za serikali bara na zanzibar. zanzibar na tanzania kwa ujumla zimepata fursa za kutangaza sekta ya utalii, uchumi wa viumbe wa baharini na utamaduni wa zanzibar ambayo itatoa nafasi kubwa ya kuvutia wawekezaji wa viwanda vya kuongeza thamani katika sekta ya viungo kama karafuu, mwani, chumvi, dagaa na kuendeleza miundombinu ya uchumi wa zanzibar.