BALOZI SEIF AMELIPONGEZA ZBC KWA KUENDELEZA MASHINDANO YA VIJANA YA KUWANIA KOMBE LA MAPINDUZI

Makamo wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi amelipongeza shirika la utangazaji zanzibar zbc kwa kuendeleza mashindano ya vijana ya kuwania kombe la mapinduzi (zbc watoto mapinduzi cup).
amesema kuwepo kwa mashindano hayo kumeweza kutoa fursa kwa vijana kuonyesha vipaji vyao pamoja na kuyaenzi na kufahamu lengo la mapinduzi ya zanzibar.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa vya mashindano hayo kutoka kwa mfanyabiashara maarufu mohd raza balozi seif amesema zanzibar kuna vipaji vingi vya vijana ambavyo ikiwa vitaendelezwa itakuwa hazina ya nchi.
Amefahamisha kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau na wadhamini ili kuhakikisha zanzibar inajipatia sifa na kupiga hatua katika medani ya michezo nchini.
Waziri wa habari utalii, utamaduni na michezo rashid ali juma amesema wizara yake kwa kushirikiana na shirika la utangazaji itaendeleza kutoa msukumo katika mashindano hayo ili kuona vijana wanapata nafasi ya kuyaenzi mapinduzi kupitia michezo.
nae mfanyabiashara mohd raza amesema ataendelea kuiunga mkono zbc kwa kuelekeza misaada yake ili kufanikisha vyema mashindano ya watoto mapinduzi cup.
Vifaa vilivyo kabidhiwa na mfanyabiashara huyo ni pamoja na vikombe , medali, mipira, pamoja na jezi kwa kila timu zitakazoshiriki katika mshindano hayo