BALOZI SEIF AMESISITIZA KUONGEZWA UIMARISHWAJI WA MASHIRIKA YA NDEGE AFRIKA

 

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi amesisitiza kuongezwa uimarishwaji wa mashirika ya ndege afrika ili yawe kichocheo kwa kukuza usafiri wa anga sambamba na utalii.balozi seif amesema kutokana na sekta ya usafirishaji na utalii kuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi duniani mashirika hayo yaunganishe nguvu zake kuchukuwa nafasi hiyo badala ya kutegemea zaidi mashirika kutoka nje ya afrika.

balozi seif akifungua mkutano wa saba wa wadau wa sekta ya usafiri wa anga afrika kupitia shirikisho la mashirika ya ndege afrika (afraa) huko zanzibar beach resort amesema takwimu zinaonyesha kuwa ukuwaji wa usafiri wa anga pamoja na utalii vinachangia pato kubwa duniani na inatarajiwa kutoa ajira zaidi ya milioni mia nne hadi kufikia mwaka 2028.amesema zanzibar ikiwa miongoni mwa nchi hizo itanufaika zaidi endapo mashirika hayo yataimarishwa  kutokana na uchumi wake kutegemea zaidi sekta ya utalii kupitia usafiri wa anga na inachangia asilimia 27 katika pato la taifa na asilimia thamanini ya fedha za kigeni.aidha balozi seif amesema kufanyika mkutano huo zanzibar ni fursa ya kipekee kukuza uchumi ikizingatiwa zanzibar imo katika utanuzi wa uwanja wa ndege wa amani abeid karume na kuwa na matumaini ya kuongeza idadi ya watalii hasa kupitia usafirishaji wa watalii kutoka shirika la ndege tanzania.akizungumza kwa niaba ya shirika la ndege tanzania atcl mkurugenzi mwendeshaji wa shirika hilo amesema shirika limepata mafanikio katika kipindi kifupi kilichopita baada ya kupoteza umaarufu wake na sasa limeongeza hisa  zake kutoka asilimia 2 hadi thalathini na saba.