BARAZA LA MANISPAA KUHAKIKISHA UKUSANYAJI WA MAPATO UNAIMARIKA

 

Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joes Thomas amewatakka madiwani wa baraza la manispaa la mjini zanzibar kuhakikisha ukusanyaji wa mapato umaimarika ili kuliwezesha kutekeleza majimu yake kwa ufanisi mkubwa.

Akifungua kikao cha madiwani wa baraza hilo huko darajani marina amesema chombo hicho kina  kazi nyingi za kufanya  zikiwemo za usafishaji wa mji na ununuzi wa vifaa  mambo ambayo hayawezi kutekelezeka  bila ya kuwa na  fedha za kutosha.

Aidha mkuu huyo wa wilaya amehimiza kufanyiwa kazi changamoto mbali mbali zinazolikabili baraza la manispaa ikiwemo ya mirundikano ya taka katika maeneo kadhaa ya mji wa zanzibar.

Naibu mkurugenzi wa baraza hilo  ndugu ali abdalla amesema baraza linakusudia kufanya zoezi la nyumba kwa nyumba ii kubaii nyumba zisizo na vyoo pamoja na karo na kuwachukulia hatua wamiliki wake.

Akizungumzia kikao hicho naibu meya wa baraza hilo  bimkubwa saidi sukwa   amesema kina lengo la kujadili utekelezaji wa shughuli zake kwa kipindi cha miezi mitatu na kuwataka madiwani pamoja na mambo mengine kuhakikisha eneo la darajani linapendeza muda wote hasa ukizingatia ni kioo cha mji wa zanzibar.