BARAZA LA MANISPAA LA WILAYA YA MJINI LIMEPEWA MUDA WA MWEZI KUKAMILISHAU JENZI WA KITUO CHA KIJANGWANI

 

Baraza la manispaa la wilaya ya mjini limepewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha mradi wa ujenzi wa kituo cha daladala kijangwani ili kukamilisha azma ya serikali kuimarisha huduma ya usafiri.

Waziri wa ofisi ya Rais, tawala za mikoa, Serikali za mitaa na idara maalum za SMZ mh. Haji Omar Kheri ametoa agizo hilo alipotembelea eneo hilo kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi na kueleza kutorishwa na kasi ya kiutendaji ambapo viongozi wa manispaa wameahidi kuongeza kasi ili kukamilisha haraka mradi huo kwa muda walioagizwa.

Wakati huo huo Mhe Haji Omar kheri ametoa wito kwa shirika la umeme na idara ya maji kujenga utamaduni wa kutekeleza majukumu yao kwa ushirikiano ili kulinda miundo mbinu ya huduma za jamii ya maji na umeme iendelee kutumika kwa utaratibu unaokubalika kisheria.

Ametoa wito huo alipotembelea barabara ya magogoni/kinuni hadi fuoni mambo sasa na kuahidi kuwa serikali itaendelea kuimarisha huduma za jamii ikiwemo barabara.