BARAZA LA MANISPAA LIMEWAKAMATA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA KUKATA WAYA ZA UMEME

Baraza  la manispaa mjini   limewakamata watu wawili kwa tuhuma za  kukata waya  za  umeme  na kuziiba   katika maeneo ya bustani ya botaniki iliyopo migombani.fundi mkuu wa baraza la manispaa mcha abdalla mcha ameiambia zbc kwamba  wizi huo umefanyika  jana  usiku baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi wanaoishi hapo na kufanikiwa kuwakamata watu hao majira  ya saanne za asubuhi.

Amesema watu  hao ambao wako kituo cha polisi mwembe madema  wanatuhumiwa kukata waya hizo za umeme zenye ukubwa  usiopungua mita mia nneMkaazi wa maeneo hayo  ali khamis ali ameiambia zbc kwamba vitendo vya kuiba waya hizo si vya kiungwana  na kwamba vinahitaji kuchukuliwa   hatua za sheria  kwa kuhujumu huduma hiyo ya umeme ambayo ni muhimu kwa  wananchi na wapita njiaHata hivyo mwenyekiti wa jumuiya  ya  bustani ya mnara wa mbao khalifa mzee ali amesema   wizi huo  unasababishwa na watu wasiopenda maendeleo ya hapo .Kufuatia  wizi huo amelishauri baraza la manispaa kuweka vibanda vitakavyotoa huduma  kwa  wananchi  na kubaki  kwa muda wote katika maeoneo hayo.

 kuwepo kwa taa hizo kunafuatia kujitokeza kwa vitendo vya kihalifu wanavyofanyiwa wapita njia za maeneo hayo  hasa katika nyakati za usiku.