BARAZA LA MANISPAA MJINI LIMEAMUA KUWAPA MAFUZO YA SHERIA WAJUMBE WA BARAZA HILO

Baraza la manispaa mjini limeamua kuwapa mafuzo ya sheria wajumbe wa baraza hilo na watendaji wa manispaa .
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo ya sheria mkurugenzi wa manispaa mjini nd aboud serenge amesema baraza limeona ipo haja ya kuwa patia mafunzo ya sheria kwa wajumbe wake kwa sababu tofauti ikiwemo kuwa na wajumbe wapya wa baraza hilo pia kuzifahamu sheria zinazo tumika baraza la wawakilishi.
Pia amesema sheria za baraza la manispaa haziko tofauti sana na sheria za baeaza la wawakilishi.
Nd mussa kombo mshauri wa sheria baraza la wawakilishi ambaye ndio mkufunzi wa mafunzo hayo amesema vyombo hivi vinafanana katika upande wa sheria na wajumbe wake ni muhimu kuzifahamu sheria zinazo endesha chombo hicho.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha sheria baraza la manispaa mjini bi fatma haji ameyafunza mafunzo hayo kwa kusema kutokana na mfumo wa ugatuzi pamoja na mafunzo hayo waliyo yapata itakuwa sehemu nzuri sana kwao kuyatekeleza majukumu ya kuwatumikia wananchi.
Mafunzo hayo yamechuwa siku mbili katika ukumbi wa manispaa umewajumuisha wajumbe wa baraza hilo na watendaji yana endeshwa na washauri wa sheria kutoka baraza la wawakilishi