BARAZA LA MANISPAA MJINI LIMEDHAMIRIA KUYABORESHA MAENEO YA BIASHARA

 

Baraza la manispaa mjini limedhamiria kuyaboresha maeneo ya biashara yaliyochini ya usimamizi wa manispaa hiyo ili kuwawezesha wafanyabiashara na watumiaji wa maeneo hayo kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa baraza hilo nd. Saidi juma ahmada wakati akizungumza na wafanayabiashara wa soko la darajani alipokua harakati za uboreshaji wa miundombinu ya kibiashara sokoni hapo.

Mkurugenzi huyo amesema kwakutambua umuhimu wa soko hilo baraza limelenga uliboresha kwa kulipaka rangi, kuliezeka sehemu zinazovuja, kuimarisha miundo mbinu ya usambaaji wa maji safi na maji taka na kusimamia mpangilio nzuri wa bidhaa zinazouzwa katika soko hilo.

Aidha mewataka wafanyabiashra na kuonesha mashirikiano katika kuimarishausafi sokoni hapo ili kulinda haiba ya soko hilo kwa wageni na wenyeji wa mji wa zanzibar.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko hilo wamesema juhudi zinazochukuliwa na baraza la manispaa mjini katika kuboresha miundombinu ya biashara sokoni hapo ni za kupongezwa huku wakiwataka wasibweteke na maboresho hayo badala yake wafike mara kwa mara kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili.

Wafanayabiashara hao wameutaka uongozi wa baraza la manispaa mjni kubuni njia sahihi za kuwasimamia sambamba na kuweka mpangilio nzuri wa kuingia na kutoka katika sehemu zao za biashara kwa wafanayabiashra wa asubuhi na jioni wa soko hilo.

Wakati huo huo baraza la manispaa mjni limeendelea na opesheni maalumu ya kusafisha vituo vya kuhifadhia taka ndani ya mji wa zanzibar ambapo zaidi ya vituo 15 vimekaguliwa na kufanyiwa usafi maalu huku wananchi wakisisitizwa kutupa taka katika vituo sahihi vilivyowekwa ili kuepusha uzaagaji ovyo wa taka.